Saturday, January 8, 2011

MBWEMBWE ZA KU-PASS OUT MLALE JKT

OPERESHENI UZALENDO NI YA 100 toka kuanzishwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa Mwaka 1963. Mkuu wa Kikosi cha 842 KJ Mlale JKT Songea mkoani Ruvuma, Major Abas Ahmed, aliwaambia wageni waalikwa na Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara kabla ya Kufunga Mafunzo ya awali ya Kijeshi yaliyochukua miezi 6 ya kuhenya ya Operesheni hiyo.
Kwa ujumla, Mlale JKT pamoja na Vikosi vingine huandaa vijana wasichana kwa wavulana na kuwafundisha utii, maadili mema pia mbinu za Kijeshi na stadi za kazi mbalimbali tayari kwa vijana hao kushiriki ujenzi wa taifa lao. Major Abas Ahmed anasema Operesheni UZALENDO ni ya aina yake na yenye kumbukumbu kubwa hapa nchini ambayo inaonesha hatua kubwa na kazi nzuri liliyofanywa na JKT katika kuandaa vijana wenye maadili mema ya kitanzania. faidi uhondo huu ambao haukumuacha kwenye kiti Naibu waziri wala Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenister Muhagama na wageni wengine kuingia uwanjani kulisakata rhumba la Bendi ya Mapipa ya Vijana hao wa Mlale JKT, Operesheni Uzalendo wakisaidiwa na Vijana wawili tu wa Operesheni Kilimo Kwanza kuyakung'uta mapipa hayo yaliyotoa muziki murua siku ya Tarehe 7/1/2011 mliopitia JKT mpo! (Picha zote na Maelezo na Juma Nyumayo)












































1 comment: