Saturday, August 18, 2012

TANZIA

TANZIA - MWANDISHI MBOGORA AFARIKI DUNIA
Wakuu,
Habari za leo, habari za Jumamosi,
Tumepata taarifa kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwamba mmoja wa maofisa wake na Mwanahabari na Mhariri wa siku nyingi, Alfred Mbogora amefariki Dunia leo saa 11.00 alfajiri katika hosipitali ya Taifa ya Muhimbili.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajumbi Mukajanga amesema kwamba Mbogora alilazwa Muhimbili tangu Jumanne baada ya kuwa ameanguka katika eneo la Tegeta, mara baada ya kupata chakula wakiwa njiani kwenda Bagamoyo kwa shughuli za kikazi.
Kabla ya kuanguka, Mbogora alikuwa akilalamika kwamba anasikia kuishiwa nguvu kwenye mguu na mkono na alipojaribu kusimama ili kutembea kutokana na hali aliyokuwa akiisikia mwilini alianguka.
Tangu wakati huo (baada ya kuanguka) alikata kauli na hakuwa kusema chochote hadi hapo alipokata roho leo alfajiri. Ni pigo kwa sekta ya habari nchini, kumpoteza mwanahabari mwenzetu ambaye ametoa mchango mkubwa katika sekta yetu ya habari.
Inasadikiwa kwamba msiba wa Mbogora uko nyumbani kwake Segerea, lakini taarifa zaidi tutazipata kadri tutakavyoendelea kuwasiliana na MCT pamoja na familia ya marehemu.
Tunachukua fursa hii kuwapa pole wafiwa wote, kwanza ni familia ya marehemu, MCT na wanahabari wote nchini. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake luhimidiwe, Amen.--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

Thursday, August 16, 2012

Maandalizi ya Sensa, Cheki Bango

KILA  MMOJA  WETU ANAPASWA  KUSHIRIKI  SENSA AGOST 26Sensa kwa maendeleo, hivi sasa nchini Tanzania wimbo ni mmoja tu. Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa.

Majimaji yajengewa uzio

Kaimu Muhifadhi Kiongozi wa Makumbusho ya Taifa ya Mashujaa wa Majimaji Songea, Balthazar Nyamusya (Kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu alipotembelea makumbusho hayo kwa maraq ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Mkoa huo, nyuma ya Mwambungu ni Chief wa wangoni,  Emmanuel Xavery Zulu Gama.
Makumbusho haya sasa yanajengewa uzio, yanapendeza kwelikweli. Hongera Shirika la Makumbusho ya taifa kwa kazi nzuri inayosimamiwa na Bw. Balthazar Nyamusya hapa Songea.

Wednesday, July 25, 2012

Vimwana wa kingoni

Picha hii ni kwa hisani ya Blog ya VANGONI hapo ndo uvaaji wa wanawake wa kingoni wakiwa wamejipamba kisawasawa. Nimeiona picha hii imenivutia saaana nadhani pia wasomaji wetu watanuafaika na kuvuta hisia miaka hiyo ya 1900.

Salaaaam wote

Wanamtandao nawasalimia woote kabisa. Kwa sasa nipo Dar es Salaam, naendelea kufuatilia story na picha zenu asanteni saana.

Thursday, May 3, 2012

Taasisi ya Elimu Tanzania kujenga stadi za kusoma kuandika na kuhesabu (KKK)

Picha ya kwanza juu: Mkurugenzi wa Chuo kikuu Huria (OUT), Songea Andrew Komba akichangia hoja kuhusu maboresho ya mitaala ya elimu hapa nchini.


Mkurugenzi Mkuu Taasisis ya Elimu Tanzania, Dr. Paul D. Mushi akikielezea kitabu cha Tafakuri ya Maboresho ya Mitaala na Mkakati wa Mafunzo kwa Wadau katika Ukumbi wa maliasili Mjini Songea jana. (Picha na Christian Sikapundwa)

WADAU WA ELIMU WAKIPITIA CHANGAMOTO ZA ONGEZEKO LA KUTOJUA KUSOMA KUANDIKA NA KUHESABU

Kikundi cha wadau toka Manispaa na Songea Vijijini wakiibua hoja mbalimbali kuhusu mitaala ya elimu na ongezeko la wasiojua KKK kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hapa mkoani Ruvuma ili zichukuliwe na Taasisis ya elimu Tanzania -TET wazifanyie kazi kuokoa jahazi. ( Picha na Christian Sikapundwa)