Na Steven Augustino, Tunduru
VYOMBO vya Habari nchini
vimehimizwa kufuatilia na kuandika Habari za maendeleo, Changamoto na matatizo
yote yanayo vikabiri Vijiji na Wilaya zilizopo pembezoni .
Haya yalisemwa na Mkuu wa
Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho wakati akitoa taarifa ya Utekeelezaji wa
Serikali ya awamu ya Nne kupitia ilani
ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2005 /2012.
Aidha katika taarifa hiyo Dc,
Nalicho alidai kuwa endapo daraja la Vyombo vya Habari na wanahabari
hawatatembelea na kuandika taarifa hizo watakuwa hawawatendei haki wananchi wa
maeneo hayo hali ambayo itawafanya waendelee kulishwa taarifa na matukio yanayo
patikana mijini pekee.
Akifafanua taarifa hiyo Dc,
Nalicho alisema kuwa mbali na Juhudi za Serikali kupeleka Maendeleo kupitia
Sekta mbalimbali katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, bado taarifa zake
zimekuwa haziandikwi vyakutosha ikiliganishwa na maeneo mengine.
Alisema
Wilaya hiyo ambayo
ipo Pembezoni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za
kutokuwa
na Barabara za uhakika zinazo unganisha makao makuu ya Wilaya hiyo na
Mkoa wa Ruvuma mjini Songea na Wilaya ya Tunduru na Nanyumbo
Mkoani Mtwara hali ambayo imezusha malalamiko mengi hasa nyakaati za
masika.
Akizungumzia mapato ya ndani
katika halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Nalicho alisema kuwa katika kipindi hicho
Halmashauri ya Wilaya hiyo imefanikiwa kuongeza hadi kufikia Tsh.718, 018,977
.43 kutoka Tsh. 201,738,593.78 mwaka 2005 ilikuwa ni ongezeko la kiasi cha Tsh.
516,280,393.65.
Kuhusu Sekta ya Uzalishaji wa
Mazao mbali mbali ya Chakula Dc, Nalicho alisema kuwa katika kipindi hicho Wilaya imeongeza kutoka
tani 115,199 hadi tani 328,424 likiwa ni ongezeko la asilimia 169%.
Alisema hali hiyo imetokana
na Wilaya hiyo kuboresha miundo mbinu ya kujenga mifereji ya Umwagiliaji.
Kupeleka Matrekta makubwa 25 kutoka 0
mwaka 2005, Materekta madogo Powertillers 187 na pembejeo za Kilimo kutoka tani
900.65 mwaka 2005 hadi tani 6,412 mwak
2012.
Alisema upande wa Sekta ya
Mifugo Dc, Nalicho alisema kuwa Wilaya hiyo imepiga hatua kwa kuwa na ongezeko
la Ng`ombe 35,758 kutoka 2,780 mwaka 2005, Mbuzi 43,413 kutoka 18,700, Nguruwe
3,110 kutoka 406 na Kuku 310,900 kutoka 107,430 hali ambayo imewasaidia wananchi wa Wilaya hiyokuinua
vipato vyao.
Akizungumzia changamoto
mbalimbali na Mikakati yake Bw. Nalicho alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa
vikwazo hivyo Wilaya yake imekuwa ikijitahidi kukabiliana navyo ikiwa ni pamoja
na kuandaa Sheria ndogo ndogo za kukabiliana navyo.
No comments:
Post a Comment