Thursday, September 22, 2011

CHADEMA YAKACHA KUMSIMAMISHA MGOMBEA UMEYA!

Chama cha Upinzani kilichochukua Kata tano Muhimu kati ya 21 katika Manispaa ya Songea,CHADEMA kimekacha kumsimamisha Mgombea katika Uchaguzi wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Siku ya Ijumaa Septemba 23, mwaka huu kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mstahiki Meya Ali said Manya aliyefariki na Kuzikwa nyumbani kwake Lizaboni mjini hapa. Mheshimiwa Manya alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea baada ya Ushindi katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 na kuchaguliwa kuwa Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Lizaboni.
Chama cha Mapinduzi CCM ndiyo pekee kimemteua Mheshimiwa Charles muhagama Diwani wa Kata ya Matogoro kugombea Nafasi hiyo muhimu. Hivi sasa Manispaa ya Songea ipo chini ya Naibu Meya Mariam Dizumba mheshimiwa Diwani Viti maalum. Juu pichani wanaonekana Mheshimiwa Charles Muhagama (kushoto) akiteta jambo nje ya Ukumbi wa Songea Club na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Songea Mheshimiwa Ali Said Manya na Marehemu Adam Ngongi maarufu Mzee Yapenda ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya SOUWASA. Ilikuwa Julai 20, 2010 wakati wa kusaini Mkataba mkubwa wa kuendeleza Programu ya maji.

Thursday, September 8, 2011

He kumbe migogoro ya kumiliki mali ni kukosa mahusiano mema wakati wa kutafuta?


Na Juma Nyumayo, Dar es Salaam,

KUTOKANA na migogoro mingi inayoibuka katika ngazi ya kaya na familia hapa nchini kutokana na kuwa na mahusiano mabaya katika kuzalisha na kumiliki mali, familia hizo zimetakiwa kujenga na kuboresha mahusiano yao kwa kufuata vigezo vya uwazi na upendo hatua kwa hatua kabla mali wanazozalisha hazijawatesa kwa kuwagombanisha kwa kile kinachodaiwa nani mmiliki halali kati ya mwanamke na mwanamume.
Hilo ni moja ya azimio lililofikiwa na washiriki wa warsha ya Uchumi na Ukombozi wa mwanamke kimapinduzi inayoendeshwa na Chuo cha Mafunzo ya Jinsia cha TGNP katika Ukumbi wa kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha dar es Salaam.
Katika hali ya kubaini tatizo kuu la wanandoa pia familia nyingi kusambaratika kutokana na migogoro ya nani amiliki mali, au kurithi wanawarsha hao wamechambua mbinu mbalimbali na kuja na mapendekezo ambayo huenda yakapunguza tatizo linalozikabili familia nyingi hapa nchini hasa kutokana na mfumo dume unamtenga mwanamke kumiliki mali hasa zenye thamani.
Sheikh wa wilaya ya Liwale, Adam Mpelengana, alisema ni muhimu kwa wanaume wote kutambua kuwa wanawake ni wasaidizi wa mwanamume na ni jukumu la mwanamume kumpenda na kufanyia haki anazostahili badala ya kumuachia kazi nyingi bila usaidizi.
"Mwanamke anatakiwa aenziwe apendwe kwa kila namna, haifai kuendekeza mila na desturi za kumtumikisha mwanamke,' alisisitiza Sheikh Mpelengana.
Awali Mchungaji wa KKT toka Shinyanga, Odorus Gyunda , alisema ni muhimu kubainisha wazi ukatili wanaofanyiwa wanawake ni kinyume cha mapenzi ya mungu.
"imeelezwa wazi kuwa Mwanaume ampende mke wake na mwanamke amtii mumewe," alisema na kubainisha kuwa hayo hayawezekani kama hakuna upendo na mawasiliano mema katika uzalishaji na taratibu zote za kuishi.
Hata hivyo wanawarsha hao wamependekeza kuwa ili kusiwe na migogoro katika matumizi ya fedha na umiliki wa mali ni vyema wenza wakashiriki kikamilifu maamuzi ya kupanga utafutaji wa fedha au mali hatua kwa hatua mapema.
jambo jingine lililoelezwa ni wanawake na wanaume kwenye kaya zinazotegemea kilimo wajue mahitaji yao ya chakula mapema wakati wa kuandaa mashamba ili wasije uza chakula chote kwa tamaa ya fedha.
Wakijadili suala la kudhibiti matumizi na kuweka kumbukumbu za mapato katika ngazi ya kaya washiriki hao wamependekeza kuwe na daftari la pamoja la kuwekea kumbukumbu za mapato na matumizi katika kila hatua.
Aidha wamewaasa wanawake kuwa makini na mchango wa nguvu kazi zao katika kuhudumia familia pia kuzalisha mali katika kaya na kuhoji matumizi na shughuli za kila mmoja katika kaya husika.
Vilevile imeelezwa wazi kuwa usafi na kujali afya za wanafamilia ni mtaji mkubwa katika kuleta mahusiano mema katika kutumia muda na kumiliki mali za kaya.
Washiriki hao hawakuishia hapo, walisema hayo yatawezekana iwapo, kutatengwa walao siku moja katika wiki kuzungumzia masuala na maendeleo ya kaya husika kwa kuwahusisha mume, mke na watoto ili kaya ziendeshwe kwa shughuli na bajeti zenye mtazamo wa kijinsia zaidi.
MWISHO

Wednesday, September 7, 2011

Migogoro ya ardhi ikome!


WALALAMIKIA MIGOGORO YA ARDHI KUKWAMISHA MAENDELEO

Na Juma Nyumayo, Dar es Salaam
MIGOGORO ya Ardhi inayoendelea katika mikoa mbalmbali hapa nchini imetajwa kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya wanawake katika harakati zao za kujikwamua kiuchumi pia kuleta ukombozi wa mwanamke na maendeleo stahiki hapa nchini.
Hayo yameibuliwa na washiriki wa warsha inayoendelea katika Ukumbbi wa Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa mifumo na vikwazo vinavyozuia wanawake kujikwamua kiuchumi.
Akiwasilisha Mada hiyo, Mwezeshaji toka TGNP, Rehema Mwateba alisema ni vyema washiriki wakaeleza hali halisi ya umiliki wa ardhi na migogoro inayendelea kujitokeza hivi sasa ikilinganishwa na mifumo iliyopo katika kumkomboa mwanamke kimapinduzi.
Mshiriki mmojawapo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro,Kibena Kingo, ametolea mfano wa mapigano yanayoibuka marakwa mara na yanayoendelea wilayani kwake kati ya wafugaji na wakulima, ambapo chanzo kikiwa ni matumizi ya Ardhi na kwamba mgogoro huo ni mkubwa.
Imeelezwa wafugaji hao wanaotokea mikoa ya kaskazini na kati wanalishia wanyama wao mazao ya wakulima bila kujali na hivyo kuwakwaza wananchi wewnyeji ambao wengi wao ni wakulima wa mazao ya chakula.
"Mgogoro wa ardhi ni mkubwa na waathirika wakubwa ni wanawake na watoto, hata hivyo ni lazima hatua zichukuliwe ili kutatua migogoro hii kabla hayajatokea mauaji makubwa," alishauri Kingo.
Wakati kingo akielezea mgogoro wa ardhi Morogoro bado Mwezeshaji toka TGNP Darus Badi alipaza sauti yake na kuthibitisha kuwa mtandao huo una rekodi ya migogoro ipatayo 60 ya ardhi katika mkoa huo na kwamba kuna haja ya kulichukulia uzito tatizo hilo.
" Tuna migogoro tunayoijua kule Morogoro na tukiwa kama wanaharakati lazima tushirikiane kuchukua hatua," alisema Badi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa halamashauri ya Mbinga Prisca haule alisema migogoro mingi ya ardhi huko Mbinga imeibuka kutokana na wakazi wa huko kutafuta maeneo ya kulima baada ya kuishiwa ardhi maeneo ya milimani.
"Kuna migogoro ya ardhi katika familia na nje ya familia kupigania ardhi ya kulima," alisema na kubainisha kuwa bado kuna mipango mibovu na sera isiyoeleweka katika umiliki wa ardhi.
Hata hivyo lawama azikuachwa kwa wawekezaji katika vitalu vya mbuga za wanyama hadi migodi ya madini kama ya Buzwagi, Geita hadi huko Namtumbo kwenye Urani( Uranium) ambako wananchi wa kawaida na hasa wanawake wanaona kama mchezo wa kuigiza wasijue kinachoendelea kwenye ardhi yao.
Lawama kibao zimeelekezwa pia kwa Mamlaka za vijiji na Miji kugawa ardhi kwa upendeleo na hasa kwa wale wanaotoa kitu kidogo kwaajili ya kupata viwanja vya makazi na kuwaacha kabisa wanawake nyuma.
Wakati wa Ufunguzi wa warsha hiyo, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia ya TGNP, Dkt. Diana Mwiru, aliwaasa washiriki kujadili mada mbalimbali kwa lengo la kujenga uelewa na kusaidi jamii tunapoelekea kusherehekea tamasha la Jinsia na Mika 50 tangu Tanganyika kupata Uhuru wake.
Dkt. Mwiru,alisema, katika miaka 50 iliyopita wanawake wa nchi hii wameendelea kuachwa nyuma katika kumiliki na utoaji wa maamuzi juu ya rasilimali ikiwa ni pamoja na ardhi.
Mwisho

Tuesday, September 6, 2011

TGNP yawapiga msasa Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi!


Na Juma Nyumayo, Dar es Salaam

WANAWAKE nchini wameshauriwa kuziangalia changamoto juu a uelewa wa masuala ya uchumi na ukombozi wa wanawake baada ya miaka 50 toka uhuru ambapo wanawake wengi waeachwa nyuma kielimu na kiuchumi.

Hayo yameelezwa leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia ya TGNP, Diana Mwiru, wakati wa Ufunguzi wa Warsha ya Uelewa wa Masuala ya uchumi na wanawake yanayoshirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani toka mikoa yote ya Tanzaia Bara.

Mwiru, amesema, katika miaka 50 iliyopita wanawake wa nchi hii wameendelea kuachwa nyuma katika kumiliki na utoaji wa maamuzi juu ya rasilimali.

Mkuu huyo, amebainisha kuwa wakati umefika hivi sasa kwa jamii ya kitanzania kuhakikisha maisha bora kwa kila mtanzania yaapatikana kwa kuwashirikisha watu wote kutafuta na kutumia rasilimali za taifa.

Aemesema ni muhimu wa serikali zetu kuhakikisha wananchi hasa wanawake wanashiriki katika mchakato wa bajeti na iwe na mtazamo wa kijinsia.ngi wao ni viongozi wa Dini, waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa asasi zisizo za iserikali waandishi wa Haari na wanaharakati wanawajibu wa kuhakikisha uchumi na ukomboziwa mwanamke kimapinduzi unakwenda sambama na elimuya mtoto wa kike.

Mwateba amesema mia na desturi ambazo ni vikwazo katika ukombozi huo a faa zibainishwe wazi na kwama zijengwe nguvu za pamoja katika kutetea haki za uchumi.

Katika hali nyingine washiriki wawarsha hiyo wameeleza kwa kuna mabadiliko mengi yanajitokeza hivi sasa na kwamba baadhi ya Sera na kanuni zinawakandamza wanawake katika harakati za kumkomboa

Prisca Haule, Mheshimiwa Diwani Viti Maalum halmashauri ya Mbinga alisema inashangaza kuona Diwani wa Viti maalum hana nafas kugombea uongozi wa juu kama Uenyekiti wa Halmashauri au Umeya wa Manispaa.

"Hizi sera zinatunyanasa na kutuweka nyuma a kuwa wanyonge, alisema Haule.

Kauli hiyo iliungwa Mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini Kibena Kingo kuwa hata wabunge viti Maalumu nao hawawezi kuteuliwa kupata nafasi ya Uspika au Uwaziri Mkuu.

"Hawawezi kupata nafasi kama hizo hivyo ukombozi wa mwanamke unavikwazo vingi," alisema Kingo.

Wakati vikwaz hivyo vikibainishwa, Diwani Anna Lyimo kutoka Halmashauri ya Moshi amewalalamikia wanaume wa Moshi kuwaingilia wanawake katika zao lao la Ndizi ambalo kimsingi ni zao la chakula na likimilikiwa na wanawake.

Lyimo alisema kuingiliwa huko kumetokana na kuanguka kwa zao la Kahawa na kitendo hicho kinaibua mgogoro wa kimaslahi ya kiuchumi.

Naye mwezeshaji Rehema Mwateba, alisema kuna mifumo ya kiuchumi na Matabaka ambayo bado yanamkandamiza mwanamke na hivyo washiriki ambao we

Mafunzo hayo ya siku tano yanaendelea katika Ukumbi wa Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo washiriki wanategemewa kujenga uelewa wa masuala ya uchumi na ukombozi wa waawake kimapinduzi na kuwaelewesha watoa maauzi katika maeno yao wanayotoka.

Mwisho

Sunday, September 4, 2011

Breaking Neews- Mama Kambona wa Tunduru amefariki!



MAELFU ya wakazi wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma walijitokeza kumzika mwasisi wa Tawi la Chama cha TANU katika Tarafa ya Nampungu Wilayani humo marehemu Edith Angela Kambona (73) pichani aliyefariki akiwa nyumbani kwake mtaa wa Extended Tunduru mjini. Mwandishi wetu Steven Agustino Chindiye anaeleza kuwa mume wa marehemu kambona, Mzee Jerome Kambona alimueleza kuwa mkewe alifariki ghafla usiku wa kuamkia septemba 1, mwaka huu 2011 baada ya kupatwa na homa ya shinikizo la damu.
Akisoma wasifu wa marehemu katika maziko yaliyofanyika katika makaburi yaliyopo nyumbani kwao, msemaji wa familia hiyo Emmanuel kambona alisema kuwa marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1938 alimaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi Mindu mwaka 1957 na baadae kujiunga na shule ya wasichana ya Newala Middle School kuanzia mwaka 1958/1959 na baadae kujiunga na masomo ya uuguzi katika chuo cha Tukuyu Mkoani Mbeya.
Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa baada ya kumaliza elimu hiyo pia wakati wa uhai wake, marehemu Kambona ateuliwa kuwa Mwenyekiti na muasisi wa chama cha Tanu katika Tarafa ya Nampungu kuanzia mwaka 1962 wadhifa ambao aliutumikia kipindi cha mwaka mmoja ambapo mwaka 1963 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Tunduru hadi mwaka 1969.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa mwaka 1970 marehemu Kambona aliteuliwa kuwa Katibu Tarafa na kutumikia wadhifa huo katika Tarafa za Kidodoma, Ligunga, Matemanga, Namasakata,Nampungu Wilayani Tunduru na Tarafa ya Lipalamba Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 1988.
Awali akisoma misa ya maziko ya marehemu kambona Padre Keneth Mathiani kutoka kanisa la Angalikana Tunduru aliwataka waamini wa madhehebu hayo kuzingatia maandiko ya vitabu vitakatifu ili waende kuishi maisha yenye furaha milele baada ya vifo vyao kama tuaminivyo kwamba Marehemu Kambona atapata tuzo hiyo vile aliishi kwa uadilifu wakati wote wa uhai wake.
Aidha Marehemu Kambona wakati wa uhai wake akiungana na viongozi wenzake wa wilaya ya Tunduru ndio waliofanikisha adhima ya kuondoa njaa Tunduru kwa kauli mbiu ya Kunjatu ikiwa na maana ya kuondoa njaa Tunduru ,kampeni ambayo ilipelekea wakazi wote wa Tunduru kulima mazao ya chakula ekari mbili na mazao ya biashara ekali moja chini ya uongozi wa Kasapila aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Tunduru kwa wakati huo.
Marehemu Kambona atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa taifa hili hasa katika sekta ya elimu na jamii kwani alikuwa ana ndoto kubwa ya kuwaona watu wanaelimika kwa kusoma kwa bidii na kukataza utoro mashuleni na mamba kwa watoto wa shule.
Marehemu ameacha Mgane, Watoto watatu, wajukuu 23 na vitukuu 14, mungu aiweke mahali pema peponi Roho yake, apumzike kwa amani amina.
Mwisho