Nlikuwa safarini Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara. Jambo la Kufurahisha ni kuimarishwa kwa miundombinu na Usafi wa Vituo vya mabus maarufu BUS STAND. Nikavutiwa kupiga picha hizo. Soma maelezo. PICHA YA KWANZA hapo juu ni Kituo cha Mabus pale Masasi Vijana wamejipanga na Bajaji na pikipiki zao wakingojea abiria. Picha hii nilipiga lango kuu la Kutokea Magari (Hakuna abiria wala biashara ndogondogo nilivutiwa na Mandhari ya Milima ile ya Mawe na Miti panapendeza saaana) asante Mchina. PICHA YA PILI. Kituo cha Mabus Mtwara, ni kisafi kwelikweli biashara kibao Bajaji chache na Bodaboda pia. PICHA YA TATU ni Kituo cha Mabus Lindi napo Mabus machache huingia hapo mengi hupitiliza nje kwa nje. barabara ni nzuri Biashara kwa Vijana ni kama hakuna vile waache wakimbilie Songea na Dar es Salaam kwani uhamasishaji wa kilimo cha Kundekunde, Mtama, Mbaazi na mazao mchanganyiko unahitajika kuchachamua uchumi wa huko. Kungojea majangusho ya nazi ni mapato ya watu wachache saaana haisaidii kuleta mzunguko wa fedha katika mikoa hiyo ambayo inalia na ukosefu wa soko la Korosho.
Pages
▼
Thursday, January 17, 2013
Haya Masasi, Nyangao Mtama, Lindi Hadi 'Ntwara' Angalieni hapa

Wednesday, January 16, 2013
Mti uliopandwa na Mhe. Rashid Mfaume Kawawa unavyoipamba Ofisi ya CCM Mkoa
Picha za hapo juu, Ni za Mti na Jengo la CCM Mkoa wa Ruvuma lililopo Barabara ya Sokoine Manispaa ya Songea.
Mti wenyewe "TECTONA GRANDS" Mzuri sana kwa kivuli, Unapendezesha jengo hilo la CCM mkoa na watu hupumzika na kuegesha magari yao hapo. Ulipandwa siku ya Tarehe 28/6/1974 na Mhe. Rashid Mfaume Kawawa aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania (Hivi sasa ni Marehemu) Tuzienzi juhudi za kupanda miti kutunza mazingira, usafi wa halki ya hewa pia Kumbukumbu za matukio na miaka. Wewe umepanda miti mingapi ya Kivuli, Matunda au Maua mwaka huu?

POKEA ZAWADI YA KALENDA
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma, Bw. Shaaban omar {Kulia) akimkabidhi Kalenda kubwa ya Ukutani ya Mwaka 2013 Mwandishi wa Habari, Bw. Gideon Mwakanosya (Kushoto) wakati Mhasibu wa Uhamiaji Mkoa huo Assistant Inspector Baraka Msasa akiangalia.
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma inaendelea kufanya vyema kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na raia pamoja na wanahabari mkoani hapa. Mpaka sasa inaendelea kutoa elimu kwa wananchi ambao waliweza kutoa taarifa kwa watu wa usalama na Idara hiyo kwa nyakati tofauti na kuwatia mbaroni wahamiaji haramu toka nchi za Somalia, Ethiopia na Elitrea wakitoroka kuelekea South Africa.

Tuesday, January 15, 2013
KAZI NI KAZI
Kazi ni Kazi, hapa Kamera yetu imechukua picha ya Baba Ubaya akiwa kazini katika Ofisi yake Mtaa mmojawapo maarufu hapa Songea Manispaa nje tu ya Baa Maarufu ijulikanayo kwa Jina la Serengeti.
Baba Ubaya hana mchezo kwa Kung'arisha viatu vya aina zote, kushona na kurekebisha Soli yeye na Bwana Kwizombe wanategemewa sana Katika eneo hilo.
DC wa Tunduru alilia vyombo vya habari kuandika habari za vijijini na pembezoni
Na Steven Augustino, Tunduru
VYOMBO vya Habari nchini
vimehimizwa kufuatilia na kuandika Habari za maendeleo, Changamoto na matatizo
yote yanayo vikabiri Vijiji na Wilaya zilizopo pembezoni .
Haya yalisemwa na Mkuu wa
Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho wakati akitoa taarifa ya Utekeelezaji wa
Serikali ya awamu ya Nne kupitia ilani
ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2005 /2012.
Aidha katika taarifa hiyo Dc,
Nalicho alidai kuwa endapo daraja la Vyombo vya Habari na wanahabari
hawatatembelea na kuandika taarifa hizo watakuwa hawawatendei haki wananchi wa
maeneo hayo hali ambayo itawafanya waendelee kulishwa taarifa na matukio yanayo
patikana mijini pekee.
Akifafanua taarifa hiyo Dc,
Nalicho alisema kuwa mbali na Juhudi za Serikali kupeleka Maendeleo kupitia
Sekta mbalimbali katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, bado taarifa zake
zimekuwa haziandikwi vyakutosha ikiliganishwa na maeneo mengine.
Alisema
Wilaya hiyo ambayo
ipo Pembezoni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za
kutokuwa
na Barabara za uhakika zinazo unganisha makao makuu ya Wilaya hiyo na
Mkoa wa Ruvuma mjini Songea na Wilaya ya Tunduru na Nanyumbo
Mkoani Mtwara hali ambayo imezusha malalamiko mengi hasa nyakaati za
masika.
Akizungumzia mapato ya ndani
katika halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Nalicho alisema kuwa katika kipindi hicho
Halmashauri ya Wilaya hiyo imefanikiwa kuongeza hadi kufikia Tsh.718, 018,977
.43 kutoka Tsh. 201,738,593.78 mwaka 2005 ilikuwa ni ongezeko la kiasi cha Tsh.
516,280,393.65.
Kuhusu Sekta ya Uzalishaji wa
Mazao mbali mbali ya Chakula Dc, Nalicho alisema kuwa katika kipindi hicho Wilaya imeongeza kutoka
tani 115,199 hadi tani 328,424 likiwa ni ongezeko la asilimia 169%.
Alisema hali hiyo imetokana
na Wilaya hiyo kuboresha miundo mbinu ya kujenga mifereji ya Umwagiliaji.
Kupeleka Matrekta makubwa 25 kutoka 0
mwaka 2005, Materekta madogo Powertillers 187 na pembejeo za Kilimo kutoka tani
900.65 mwaka 2005 hadi tani 6,412 mwak
2012.
Alisema upande wa Sekta ya
Mifugo Dc, Nalicho alisema kuwa Wilaya hiyo imepiga hatua kwa kuwa na ongezeko
la Ng`ombe 35,758 kutoka 2,780 mwaka 2005, Mbuzi 43,413 kutoka 18,700, Nguruwe
3,110 kutoka 406 na Kuku 310,900 kutoka 107,430 hali ambayo imewasaidia wananchi wa Wilaya hiyokuinua
vipato vyao.
Akizungumzia changamoto
mbalimbali na Mikakati yake Bw. Nalicho alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa
vikwazo hivyo Wilaya yake imekuwa ikijitahidi kukabiliana navyo ikiwa ni pamoja
na kuandaa Sheria ndogo ndogo za kukabiliana navyo.
WAKULIMA TUNDURU WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA BANIO
Na Steven Augustino, Tunduru
WAKULIMA wa kijiji cha Kitanda kilichopo katika kata ya Mlingoti
Maghalibi Wilayani Tunduru Mkoani wameipongeza serikali kwa kuwajengea
miundombinu ya banio ambalo litatumika katika kilimo cha Umwagiliaji.
Wakulima hao walitoa kauli hiyo wakati walipotembelewa na mkuu wa
Wilaya hiyo Bw. Chande Nalicho alipofanya ziala ya kushitukiza ili
kujionea utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi huo unao jengwa na kampuni ya
MWANAKWEZI CORPORATION LTD zikiwa ni juhudi za Serikali ya Wilaya hiyo
kuhakikisha kuwa Miradi yote inakamirika kwa wakati.
Wakiongea kwa niaba ya Wakulima na wanakikundi wa umoja wa Wakulima wa
kijiji hicho Bw.Said Masapi na Adam Bakari walisema kuwa wanayo imani
kuwa Mradi huo ukikamirika utaweza kuwanufaisha wakulima wengi idia
kuinua vipato vyao.
Walisema Umoja huo ambao ulianzishwaq mwaka 2004 kwa kuwa na wanachama
46 na walikuwa wakipata wakati wakitumia miundombinu iliyo kuwa
ikitiririsha maji kienyeji walikuwa wakipata mavuno ya wastani wa
Magunia 25 kwa mwaka.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi huo kwa niaba
ya Afisa Kilimo wa Halmailaya hiyo Bw. Chiza Marado, Mhandiosi wa
Kilimo wa Halmashauri hiyo Eng. Ayubu Alfayo alimweleza Mkuu wa
Wilaya hiyo kuwa Mradi huo ulioanza kujenzi wake julai 27 /2012
umepangwa kukamirika na kuanza kazi Mai10 mwaka huu.
Eng. Alfayo aliendelea kufafanua kuwa hadi kukamirika kwa mradi huo
utaghalimu Jumla ya Shilingi Milioni 323,157,876 na kwamba kati ya
fedha hizo asilimia 20% zimechangiwa na wananchi wa Kijiji hicho
pamoja na Nguvu kazi.
Alisema baada ya kukamirika kwa mradi huo utaweza kumwagilia eneo
lenye ukubwa wa Hekta 150 na kwa utasaidia kuongeza Mavuno kwa
wasitani wa tani 480 na kuiwezesha halmashauri hiyo kuongeza kipato
kupitiua ushuru ambao hukusanywa kupitia mazao machnganyiko.
Adha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho pamoja na kuwahimiza
wakulima hao kutunza miundombinu hiyo pia aliwaasa kuendele kuzipokea
na kuzitumia fulsa zote zinazo tolewa na Serikali ili kujiondolea rero
zinazo wakabiri.
Dc, Naliocho aliendelea kueleza kuwa kujituma pekee ndiko kutakako
wakombo na kwamba endapo wataendelea kukaa vijiweni na kusikiliza
maneno ya Upinzani kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijafanya
kitu watakuwa hawaitendei haki saerikali yao.
Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na afisa Kilimo wa Wilaya ya tunduru
Bw.Chiza marando alisema kuwa Uzalishaji wa Mazao mbali mbali ya
Chakula umeongeza kutoka tani
115,199 mwaka 2005 / 2012 hadi kufikia tani 328,424 likiwa ni
ongezeko la asilimia 169%.
Bw. Marando aliendelea kueleza kuwa hali hiyo imetokana na Wilaya hiyo
kuboresha miundo mbinu ya kujenga mifereji na mabanio ya Umwagiliaji.
Kupeleka Matrekta makubwa 25 kutoka 0 mwaka 2005, Materekta madogo
Powertillers 187 na pembejeo za Kilimokutoka tani 900.65 mwaka 2005
hadi tani 6,412 mwaka 2012.
Mwisho

Kaimu Mkuu wa Mkoa afagilia mfumo imara wa SACCOS
Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma, Joseph Joseph Mkirikiti (Pichani Kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa UWAMAVIRU) Bwana Mkirikiti amewaagiza maafisa wa Ushirika kusimamia SACCOS zilizochanga ili kukuza SACCOS hizo ili kuimarisha uchumi wa watu wa mkoa wa Ruvuma.Amesema kitendo cha maafisa ushirika kukaa ofisini tu haisaidiii kuimarisha Taasisi hizo ambazo zitajenga nguvu ya wananchi katika kuujenga uchumi.
Amesisitiza nwanawake wengi wajiunge na SACCOS wakope na kuzalisha zaidi. Amesema kitendo cha Mume kumuita mke wake mama wa nyumbani ni kashfa kubwa na yafaa kurekebisha hilo.
Amemuagiza Afisa Ushirika wa Mjini Songea kuhakikisha anaitunza SACCOS hiyo kama ng'ombe wake anayehitaji kulishwa na kukamuliwa maziwa.
Awali Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye aliwahi kuwa Meneja wa SACCOS kutoa ushuhuda wa jinsi alivyoweza kusaidia watu wa chini kuwa wa kati na wakati kusonga juu katika kukuza vipato vyao kwa kuangalia vigezo kwa wanachama katika kukopa kwa wanachama na kufikia malengo yao kwa muda muafaka.
"Nimekemea kitendo cha watu kukopesha kwa watu kukaaa chemba na kuuliza ukikopeshwa zangu ngapi/" alikemea tendo hilo.
.
UWAMAVIRU SACCOS wafanya mkutano wa mwaka
Umoja wa Wanunuzi Mazao Vijijini Mkoa wa Ruvuma SACCOS (UWAMAVIRU) wafanya mkutano wao wa Mwaka katika Ukumbi wa SACCOS ya Walimu Songea. Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye amekasimu madaraka hayo kwa Mkuu wa wilaya ya Songea, Bw Joseph Joseph Mkirikiti. (Pichani toka Kushoto ni Makamu mMwenyekiti wa SACCOS hiyo Bw. Thadey Mwakaguo, Katikati Mwenyekiti Bw. Ernest Malyatabu na Meneja wao Bw. Dokuta Nditti) Tutawaletea yatakayojiri.
HERI YA MWAKA 2013
HERI YA MWAKA MPYA WASOMAJI WA BLOG HII. READERS OF THIS BLOG, HAPPY NEW YEAR. I WISH YOU ALL THE BEST.