Pages

Thursday, January 17, 2013

Haya Masasi, Nyangao Mtama, Lindi Hadi 'Ntwara' Angalieni hapa



Nlikuwa safarini Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara. Jambo la Kufurahisha ni kuimarishwa kwa miundombinu na Usafi wa Vituo vya mabus maarufu BUS STAND. Nikavutiwa kupiga picha hizo. Soma maelezo. PICHA YA KWANZA hapo juu ni Kituo cha Mabus pale Masasi Vijana wamejipanga na Bajaji na pikipiki zao wakingojea abiria. Picha hii nilipiga lango kuu la Kutokea Magari (Hakuna abiria wala biashara ndogondogo nilivutiwa na Mandhari ya Milima ile ya Mawe na Miti panapendeza saaana) asante Mchina. PICHA YA PILI. Kituo cha Mabus Mtwara, ni kisafi kwelikweli biashara kibao Bajaji chache na Bodaboda pia. PICHA YA TATU ni Kituo cha Mabus Lindi napo Mabus machache huingia hapo mengi hupitiliza nje kwa nje. barabara ni nzuri Biashara kwa Vijana ni kama hakuna vile waache wakimbilie Songea na Dar es Salaam kwani uhamasishaji wa kilimo cha Kundekunde, Mtama, Mbaazi na mazao mchanganyiko unahitajika kuchachamua uchumi wa huko. Kungojea majangusho ya nazi ni mapato ya watu wachache saaana haisaidii kuleta mzunguko wa fedha katika mikoa hiyo ambayo inalia na ukosefu wa soko la Korosho.

No comments:

Post a Comment