Pages

Tuesday, January 15, 2013

WAKULIMA TUNDURU WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA BANIO

Na  Steven Augustino, Tunduru
WAKULIMA wa kijiji cha Kitanda kilichopo katika kata ya Mlingoti
Maghalibi Wilayani Tunduru Mkoani wameipongeza serikali kwa kuwajengea
miundombinu ya banio ambalo litatumika katika kilimo cha Umwagiliaji.

Wakulima hao walitoa kauli hiyo wakati walipotembelewa na mkuu wa
Wilaya hiyo Bw. Chande Nalicho alipofanya ziala ya kushitukiza ili
kujionea utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi huo unao jengwa na kampuni ya
MWANAKWEZI CORPORATION LTD zikiwa ni juhudi za Serikali ya Wilaya hiyo
kuhakikisha kuwa Miradi yote inakamirika kwa wakati.
Wakiongea kwa niaba ya Wakulima na wanakikundi wa umoja wa Wakulima wa
kijiji hicho Bw.Said Masapi na Adam Bakari walisema kuwa wanayo imani
kuwa Mradi huo ukikamirika utaweza kuwanufaisha wakulima wengi idia
kuinua vipato vyao.

Walisema Umoja huo ambao ulianzishwaq mwaka 2004 kwa kuwa na wanachama
46 na walikuwa wakipata wakati wakitumia miundombinu iliyo kuwa
ikitiririsha maji kienyeji walikuwa wakipata mavuno ya wastani wa
Magunia 25 kwa mwaka.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi huo kwa niaba
ya Afisa Kilimo wa Halmailaya hiyo Bw. Chiza Marado, Mhandiosi wa
Kilimo wa Halmashauri hiyo Eng. Ayubu Alfayo alimweleza  Mkuu wa
Wilaya hiyo kuwa Mradi huo ulioanza kujenzi wake julai 27 /2012
umepangwa kukamirika na kuanza kazi Mai10 mwaka huu.

Eng. Alfayo aliendelea kufafanua kuwa hadi kukamirika kwa mradi huo
utaghalimu Jumla ya Shilingi Milioni 323,157,876 na kwamba kati ya
fedha hizo asilimia 20% zimechangiwa na wananchi wa Kijiji hicho
pamoja na Nguvu kazi.

Alisema baada ya kukamirika kwa mradi huo utaweza kumwagilia eneo
lenye ukubwa wa Hekta 150 na kwa utasaidia kuongeza Mavuno kwa
wasitani wa tani 480 na kuiwezesha halmashauri hiyo kuongeza kipato
kupitiua ushuru ambao hukusanywa kupitia mazao machnganyiko.

Adha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho pamoja na kuwahimiza
wakulima hao kutunza miundombinu hiyo pia aliwaasa kuendele kuzipokea
na kuzitumia fulsa zote zinazo tolewa na Serikali ili kujiondolea rero
zinazo wakabiri.
Dc, Naliocho aliendelea kueleza kuwa kujituma pekee ndiko kutakako
wakombo na kwamba endapo wataendelea kukaa vijiweni na kusikiliza
maneno ya Upinzani kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijafanya
kitu watakuwa hawaitendei haki saerikali yao.
Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na afisa Kilimo wa Wilaya ya tunduru
Bw.Chiza marando alisema kuwa  Uzalishaji wa Mazao mbali mbali ya
Chakula umeongeza kutoka tani
115,199  mwaka 2005 / 2012 hadi kufikia  tani 328,424 likiwa ni
ongezeko la asilimia 169%.

Bw. Marando aliendelea kueleza kuwa hali hiyo imetokana na Wilaya hiyo
kuboresha miundo mbinu ya kujenga mifereji na mabanio ya Umwagiliaji.
Kupeleka Matrekta makubwa  25 kutoka 0 mwaka 2005, Materekta madogo
Powertillers 187 na pembejeo za Kilimokutoka tani 900.65 mwaka 2005
hadi tani 6,412 mwaka 2012.

Mwisho

No comments:

Post a Comment