Pages

Tuesday, January 15, 2013

Kaimu Mkuu wa Mkoa afagilia mfumo imara wa SACCOS

Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma, Joseph Joseph Mkirikiti (Pichani Kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa UWAMAVIRU) Bwana Mkirikiti amewaagiza maafisa wa Ushirika kusimamia SACCOS zilizochanga ili kukuza SACCOS hizo ili kuimarisha uchumi wa watu wa mkoa wa Ruvuma.
Amesema kitendo cha maafisa ushirika kukaa ofisini tu haisaidiii kuimarisha Taasisi hizo ambazo zitajenga nguvu ya wananchi katika kuujenga uchumi.
Amesisitiza nwanawake wengi wajiunge na SACCOS wakope na kuzalisha zaidi. Amesema kitendo cha Mume kumuita mke wake mama wa nyumbani ni kashfa kubwa na yafaa kurekebisha hilo.
Amemuagiza Afisa Ushirika wa Mjini Songea kuhakikisha anaitunza SACCOS hiyo kama ng'ombe wake anayehitaji kulishwa na kukamuliwa maziwa.
Awali Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye aliwahi kuwa Meneja wa SACCOS kutoa ushuhuda wa jinsi alivyoweza kusaidia watu wa chini kuwa wa kati na wakati kusonga juu katika kukuza vipato vyao kwa kuangalia vigezo kwa wanachama katika kukopa kwa wanachama na kufikia malengo yao kwa muda muafaka.
"Nimekemea kitendo cha watu kukopesha kwa watu kukaaa chemba na kuuliza ukikopeshwa zangu ngapi/" alikemea tendo hilo.
  .

No comments:

Post a Comment