Pages

Saturday, June 1, 2013

NMB NAO KATIKA MAADHIMISHO YA 17 WIKI YA KUNYWA MAZIWA NA PROMOSHENI YA JISEVIE


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea, Rehema Nassibu   (kulia) na Bw. Erick Mbise (katikati) wakimsikiliza kwa makini Bw. Barnabas Haule mmoja wa watu waliotembelea banda la NMB  katika viwanja vya Manispaa ya Songea, wakati wa kilele cha maadhimisho ya 17 ya Wiki ya  Kunywa Maziwa nchini Songea mkoani Ruvuma leo (1.6.2013)



Bw. Barnabas Haule amekwisha elewa maelezo ya Huduma za kibenki karibu yako zaidi kama ya Jisevie na anajioredhesha kwa huduma hiyo ambayo ina faida za kutohitaji kuwa na fedha taslimu, kutohitaji kwenda kwenye tawi lolote la NMB ili kuweka fedha katika akaunti yako, kulipia huduma mbalimbali bila kutumia fedha taslimu. Faida nyingine kuweka fedha popote ulipo katika akaunti yako  kwa M-Pesa. Kutuma fedha kwa NMB mobile kwenda M-Pesa na Kupata huduma ya kupitia NMB ATM zaidi ya 450 nchi nzima. (Picha na Maelezo na Juma Nyumayo)



Watu wanaendelea kupewa maelekezo


Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakiendelea kutoa burudani ya ngonjera katika viwanja vya Manispaa ya Songea wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 17 ya wiki ya kuhamasisha kunywa maziwa nchini, ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt Emmanuel Nchimbi. 











No comments:

Post a Comment