Pages

Tuesday, April 9, 2013

Chuo Kikuu St Agustino (SAUT) Tawi la Songea wasisitiza Taaluma, maadili, nidhamu ya mavazi na Utendaji.

CHUO Kikuu cha St. Agustino SAUT, tawi la Songea lenye wanafunzi wapatao 629 kimejipanga vyema kutoa taaluma, na kusimamia maadili mema ili kuleta ufanisi katika kuendesha shughuli za elimu chuoni hapo.
Akizungumza leo kwa njia ya Simu na Blogu hii, Dean of Student, Michael Sinyenga, alisema Uongozi wa Chuo hicho Unatilia mkazo mambo ya maadili na hivyo wamekwisha waelekeza wanachuo na wafanyakazi wao namna wanavyotarajia kuhusu  mavazi, na mwenendo mzima wa wanafunzi wawapo Chuoni na nje ya chuo . "Tutawaangalia hasa kwenye mavazi na matendo yao  Chuoni na nje ya Chuo," alisema Sinyenga. Hivi sasa Manispaa ya Songea na Vitongoji vyake vimechangamka kibiashara na inategemewa mabadiliko makubwa yatakuja kwa mahitaji mbalimbali wakati Chuo hicho kitakapodahili wanafunzi wengi zaidi. Mahitaji hayo ni pamoja na nyumba za kupangisha wanafunzi na watumishi wa Chuo, wawekezaji na wafanyabiashara watakaohamia kufuata soko la Idadi ya watu wanaoongezeka katika mji wa Songea uliopo kusini mwa Tanzania mpakani na nchi ya Msumbiji.

No comments:

Post a Comment