Pages

Tuesday, April 9, 2013

Rais Kikwete apokelewa kwa shangwe Kasarani , Mayowe ya CCM, CCM Oyee

 Na Juma Nyumayo, Live kwenye Screen ya K 24 TV ya Kenya.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amepokelewa kwa shngwe na kusalimiana na rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuapishwa kwake. Uwanja wa kasarani umbao ulibeba wananchi na watazamaji zaidi ya elfu 60 Rais Kikwete akiongozana na Mkewe mama Salma Kikwete walishangiliwa sana kwani aliwasili uwanjani hapo baada ya Kuw3asili Uhuru Kenyatta, Rais Mwingine aliyeshangiliwa zaidi ni Rais Robert Mugabe wa Zambia ambaye naye kama kawaida yake alinyoosha mkono wake wa kulia na kufunga ngumi akishangilia.
Maandalizi hayo ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa nne wa Kenya yamehudhuriwa na  marais, mabalozi, na watu mashuhuri katika Dunia.
Hivi sasa anasubiriwa Rais wa Kenya anayekabidhi madaraka kwa UHURU Kenyata naye si Mwingine bali ni Rais wa tatu Mwai Kibaki..... Tutaendelea kuwajuza zaidi

No comments:

Post a Comment