Pages

Friday, July 12, 2013

MAAFISA WAHALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA WATEMBELEA TUJIFUNZE

Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, (Kutoka kushoto) Mweka hazina Bw. Stephen Sindagulu, Mhasibu,  Bw. David Mkande na Mhasibu, Bw Joseph Mazito. na hapo chini pia leo katika ofisi ya Tujifunze Songea



MAAFISA wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, wmetembelea Kituo cha Uchapaji (Rural Press Songea) ambacho ni Kituo cha Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini yenye makao makuu yake Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kwa lengo la kujifunza na kuimarisha uhusiano wa kituo hicho na Halmashauri ya wilaya ya Mbinga.
Kiongozi wa Ziara hiyo fupi ya Maofisa watatu, Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Bw. Stephen Sindagulu, amesema imekuwa ya mafanikio makakubwa kwani wameweza kujionea mahali kazi zao zinapochapwa na kuzungumza na uongozi wake na kuona mitambo iliyopo kiwandani hapo.

Akiwa ameongozana na Wahasibu wawili toka Ofisi yake, Bw. David Mkande na Bw. Joseph Mazito, Mweka Hazina huyo, Bw. Sindagulu, alipata kuziona baadhi ya mashine na kazi zinazofanywa pia kukagua aina mbalimbali ya karatasi kulingana na mahitaji ya wateja kuzihitaji kuchapiwa kazi zao.
 
 Kazi zinazochapwa na Kituo hicho cha Magazeti vijijini Kanda ya Kusini, licha ya kuchapisha Gazeti la Kanda ya Kusini, Tujifunze, huchapa pia   nyaraka mbalimbali za kiserikali za Sekta ya Elimu katika kunyanyua ubora  wa taaluma katika shule za msingi, sekondari na vyuo pia Idara nyingine kama Afya, Kilimo, Utawala na nyinginezo.

Huchapisha pia vitu  mbalimbali  vya watu binafsi na serikali kwa maagizo wayatakayo ikiwa ni pamoja na vitabu vya risiti, tiketi za kusafiria,  stakabadhi za malipo mbalimbali ikiwa ni pampja na fomu za malipo kama TFN 4 na 5.
Mhariri wa Tujifunze, Bw Christian Sikapundwa, ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Mbinga kwa kutembelea Kituo chake na kusema ni mfano wa kuigwa na Halmashauri nyingine katika Kanda ya Kusini.
"Ziara yenu fupi ya kuona kazi zenu huchapwa wapi na kwa ubora gani imepokelewa vizuri, na tunaamini wengine watafuata nyayo zenu,' alisema Bw. Sikapundwa.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inaendeleza uhusiano mwema uliojengeka na Kituo chake toka Enzi ya Mweka hazina wa halmashauri hiyo ambaye sasa amepanda hadi kuwa Katibu Mkuu mmojawapo katika Serikali ya awamu ya Nne , Bw. Rashid Katanga.


 

No comments:

Post a Comment