Pages

Thursday, July 11, 2013

ENEO LA MSHANGANO MANISPAA YA SONGEA LAPANDA THAMANI


Moja ya Barabara kubwa zinazochongwa katika mitaa eneo la Mshangano ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Upimaji wa Viwanja 18,000 unaofanywa na Kampuni Binafsi ya Ardhi Plan Ltd ya Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Bw. Gombo Simanditto, ili kurasmisha makazi na kuwafanya wananchi wajenge nyumba bora na kulinda usafi wa mazingira.

 
 

Hii ni moja ya barabara iliyochongwa katika eneo hilo pia, nyumba zinazoonekana kwa mbali ni eneo la Msamala kwa Gassa Manispaa ya Songea.

 

Baadhi ya  vibarua wa Kampuni ya Ardhi Plan Ltd ya Dar es Salaam wakipanga "Mawe yenye namba" Beacons tayari kwa kupanda katika viwanja vilivyopimwa rasmi mkawaajili ya makazi bora ya watu huko eneo la Misufini Mtaa wa Namanyigu ambapo zoezi hilo linakwenda sambamba na uchongaji barabara za mitaa leo.


Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mshangano Manispaa ya Songea, Faustine Mhagama akionyesha njia za mwanzo kuchongwa ili kuimarisha miundombinu ya barabara  Kata ya Mshangano, Songea.


MRADI waKurasmisha makazi na kupima Viwanja 18,000 katika mashamba na baadhi ya nyumba ambazo zilijengwa kiholela maeneo ya Mitaa ya Namanyigu, Mshangano na Muumbezi Kata ya Mshangano manispaa ya Songea umekuwa wa mafanikio makubwa na kuleta sura mpya ya kata hiyo.

Mafanikio hayo ni pamoja na watu wa kawaida, viongozi na wamiliki wa maeneo kutambua umuhimu wa upimaji baada ya eneo hilo sasa viwanja vyake kupanda thamani ghafla na kuwa kimbilio la watu wengi kutaka kujenga.

Licha ya watui wengi kukimbilia eneo la Kata ya Mshangano, mradi huo umeboresha kwa kiasi kikubwa miundombinu ya barabara ambazo hivi sasa zinaendelea kuchongwa katika Mtaa wa namanyigu na kuwafanya watu waione ramani halisi iliyochorwa katika karatasi ardhini.

Watu kadhaa waliohojiwa wameufurahia mpango huo na kusema kitendo cha kampuni ya Ardhi Plan Ltd toka Dar es Salaam kutekeleza ahadi yake kama mkataba ulivyokuwa na kuzichoinga barabara zao hawaamini na kwamba umekuwa ukombozi mkubwa.
Bw Salum Muhagama mkazi wa namanyigu, alisema hajawahi kuona kuchongwa barabara katika maeneo ya makazi kama ilivyokuwa katika mradi huo.
"huu ni ukombozi mkubwa , tangu nianze kuishi katika mji huu wa Songea sijawahi kuona utaratibu wa kuchonga barabara kama hizi," alisema Mhagama na kutolea mifano ya maeneo ya making'inda, Mkuzo, Msamala kwa gasa na hata mateka hawakuwahi kuzichonga barabara.

Viwanja hivyo 18,000 vilivyopimwa na kampuni Binafsi ya Ardhi Plan Ltd ya dar es Salaam ndiyo mradi wa kwanza wa aina yake hapa mkoani Ruvuma kushirikisha wananchi ambao waliiajiri kampuni Binafsi kupima viwanja na kuwa mfano wa kuigwa.
Kampuni hiyo ilipima viwanja vingi kwa wakati kurasmisha makazi bila kuwaondoa wenye ardhi/mashamba yao kwa kuwalipa fidia zisizokwenda na bei ya soko kama walivyofanya halamashauri ya manispaa ya Songea katika eneo la namanyigu katika Mradi uliokula Shilingi Milioni 80 bila kuchonga barabara hata moja.
Mradi huo ambao umeleta maendeleo ya makubwa na ya haraka katani Mshangano uliwhi kuleta sintofahamu kiasi kwamba Diwani wa kata hiyo Bw Faustine Muhagama aliwekwa ndani kituo cha polisi cha kati Mjini Songea kwa kupigia debe mradi huo ambao ulipata upinzani mkubwa.

Mafanikio ya Mradi huo yaliyoletwa kwa pamoja kati ya Wananchi wa Mitaaa Mitatu ya Mitendewawa, Mshangano na Namanyigu  kata ya Mshangano yamekuwa mfano bora wa utawala bora katika kudhibiti maliasili ardhi iliyomkuwa ikimilikiwa toka enzi za mababu kwa na kukubalika na Sera ya maendeleo ya Ardhi hapa nchini.


No comments:

Post a Comment