Pages

Tuesday, June 11, 2013

ZIARA YA KUKATA NA SHOKA, FIVE STAR MODERN TAARABU KUTIKISA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI


K
Marietha Msembele  akifurahia jambo

Marietha Msembele akiwa na Bint yake Tuse wakati wa maandalizi ya ujio wa Five Star Modern Taarabu , Songea
 WASANII wa Muziki wa Taarabu wa Kundi la FIVE STAR MODERN TAARABU wanatazamiwa kuitembelea mikoa ya Nyanda za juu kusini wakianzia na Mkoa wa Ruvuma mwishoni mwa mwezi Juni, 2013. Imefahamika.

Mmoja wa Maafisa wanaoshughulikia Ziara hiyo ya aina yake ya kuwatumbuiza wananchi wa mikoa hiyo ambayo sasa wapo katika mavuno, Marietha Msembele,  amesema Kundi zima lililojipanga kisawasawa kuwapagawisha wananchi wa mikoa ya nyanda za juu kusini lipo tayari na mipango ya safari yao imeiva.

Msembele amesema hivi sasa tayari wamekamilisha mipango ya ziara ya Mkoa wa Ruvuma wakianzia na wilaya za Songea na Mbinga.

"Tutaanzia hapa Songea Manispaa baadaye Mbinga na Mipango mingine tutawaambia kulingana na mahitaji," alisema Msembele  huku akifurahia ujuzi wa kundi hilo ambalo sasa limesukwa upya.

Alipoulizwa kuhusu Ratiba, Msembele alisema ratiba imetulia nakwamba amemshukuru sana, Mrs Selina Koka, Mkurugenzi wa AKO Catering ya Dar es Salaam, ambaye ni mlezi wa kundi hil;o kukubali kulileta kundi hilo kuwaburudisha wananchi wa mikoa hii.
Msembele alisema hivi sasa amekubaliwa Ukumbi wa Familia Parokia ya Bombambili, Manispaa ya Songea kutumbuiza tarehe 28/6/2013 na ule wa Ngurudoto wilayani Mbinga Tarehe 29/6/2013 ambako watu wataserebuka watakavyo.

No comments:

Post a Comment