Pages

Monday, June 10, 2013

MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MATONYA ASAKWA KAMA SUNGURA AKAMATWA ABURUZWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UTAPELI, SONGEA

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8JkmmSO8j9aQruwihAw4PCDo1JCjX9ME0Kh5vJhYE7ozgvyNRC9exInnfmaLXbwn0fxV9ey9CP-fQzXRtZwCqiUzIinM76YoFIqJWkejeZ_TBgoiDZe9BRG3XEjBjKVHBVCjO52XzkicQ/s1600/Matonya.jpg
Msanii huyo amekamatwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Baada ya kuja ukumbini akiwa amelewa hali iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbini hapo, Ndipo waandaaji wa show hiyo walipo amua ifanyike siku iliyofuatia na kiingilo kiwe ni  kununua bia tu .


Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show nyingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurejea kwake, Dar es Salaam , Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfuata hadi alipofikia nakukuta amehamia sehemu nyingine. 
 

Waandaji hao waliamua kuchukua hatua ya kumvizia katika Bus ndipo alipokamatwa , Hadi sasa yupo mahakama ya mwanzo , Taarifa zaidi  tutawaletea
 
via/ demashonews blog

No comments:

Post a Comment