Pages

Saturday, June 8, 2013

SHEREHE ZA KIPAIMARA ZATIKISA MANISPAA YA SONGEA


Misa ya Sherehe za Kipaimara zimefanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Kuu la Songea la Mt. Mathias  Kalemba Mulumba, lililopo Manispaa ya Songea leo hapo baadhi ya waumini na vijana wao wakitoka kanisani.  

 

Waumini na vijana wao wakitoka Kanisani kwa makundi wakiimba nyimbo, vigeregere, vifijo na nderemo.
 
Ni mwendo wa pikipiki, magari madogo na daldala kuwachukua watu kuelekea sehemu mbalimbali katika Manispaa ya Songea kwa tafrija na kupokea majamanda. Hapa wote waliopokea kipaimara ni wanafunzi wa Darasa la Sita toka Shule za Msingi zilizopo Manispaa ya Songea wakiwa wamevalia Sare zao za Shule ya Msingi, Kwa wale wanaosoma Shule za serikali ni Mashati meupe na Sketi au Kaptura ya Bluu wakati wale wanaosoma Shule za binafsi ni mashati meupe  pia Sketi na Kaptura hutegemea. (Picha na Juma Nyumayo)
 

Angalia hapo kwa ndani, na maandishi yanayosomeka," Kristu Jana, Leo,  Daima na Milele"
 
 

 
 
 
Haya nderemo na vifijo vikiendelea ndani ya viwanja vya Kanisa kuelekea nje kupata usafiri kuelekea majumbani. Usafiri huo ikiwa ni kwa miguu sawa, kwa pikipiki twende, kwa gari hayaaa kwa daladala mwendo mdundo  ili mradi kusafiri kwa shangwe tu. (Picha na maelezo na Juma Nyumayo)


 
Ni mwendo wa kuwahi mapokezi.

No comments:

Post a Comment