Pages

Saturday, June 8, 2013

MBWEMBWE ZA MAHAFALI CHUO KIKUU HURIA (OUT) TAWI LA RUVUMA

Rais wa Wanachuo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)  Kituo cha Ruvuma, Bw. Christian Haule,(kulia) akisisitiza jambo kwa  Mkufunzi wa chuo hicho mkoani hapa wakati wa maandamano kuelekea Ukumbi wa Chuo hicho wakitokea Ofisi za Mkuu wa Wilaya Songea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mahafalli yao leo (8/6/2013)  (Picha na Juma Nyumayo) 


Rais Haule, amewaomba watumishi wa serikali, mashirika ya umma na binafsi pamoja na wajasiliamali  mkoani Ruvuma, kusoma katika Chuo hicho kwa faida kuu  mbili. amezitaja faida hizo kuwa ni kuendelea na kazi wakiwa wanajisomea na faida ya pili kupungua kwa muda wa kupata shahada ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Hivi  chuo hicho hutoa shahada kama vyuo vikuu vingine miaka 3, ambapo awali mtu aliweza kupata shahada kwa kipindi zaidi ya hapo.
 
 
 
Brass Band ikiongoza maandamano ya Wahitimu kuelekea Ukumbini Chuo Kikuu Huriao Tanzania Kituo cha Ruvuma
Mwalimu Kikwape wa Sekondari ya Msamala Manispaa ya Songea na Mwl. Masesa (Mrs Masesa) ni miongoni mwa wahitimu wa OUT  tawi la Ruvuma na walionekana hivyo  wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano kuelekea kwenye eneo la Mahafali yao ambayo mgeni rasmi alialikwa Bahati Chale ambaye alikuwa mwanzilishi wa OUT Kituo  cha Mkoa Ruvuma
Madam Ngwai (Mrs Masesa) katika pozi la kuvaa joho
Maandamano hayoooo! kuelekea Ukumbi wa Sherehe za Mahafali hayo ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Kituo cha Ruvuma yakitokea jingo la NSSF Manispa ya Songea leo (Picha na Juma Nyumayo)
Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria  cha Tanzania Kituo cha Ruvuma, Christian Haule (katikati) akiongoza Maandamano kuelekea Ukumbi wa Mahafali ya wahitimu 81 wa OUT mkoani hapa leo 8/6/2013 ( Picha zote na Juma Nyumayo)

Mtumishi wa SOUWASA Bw Kinyangazi naye ni miongoni mwa wahitimu akifurahia kazi nzuri ya kupiga kitabu akiwa kazini.


No comments:

Post a Comment