Pages

Wednesday, June 19, 2013

SAFARI YA LIULI YATUFUMBUA MACHO KUHUSU VYOMBO VYA USAFIRI


"WE ACHA TU" "FORCE" ni Maneno yaliyoandikwa katika Bus hilo la SADI liendalo Mbambabay hadi Liuli likitokea Songea. Usafiri Murua kabisa na hao uwaonao ni Dereva(kushoto) na Kondakta   huyo dada, ni wakarimu sana kila mtu wanamuita mjomba. Hongera sana SADI Bus service. picha hiyo nilipiga eneom la Gereza la Kita wilaya ya Mbinga "we acha tu"

PRIDE OF NYASA "ZIKOMO KWA MBILI" hilo ni Bus la Kisumapai linalofanya safari zake toka Songea hadi Liuli-Nyasa eneo lenye utalii na fukwe nzuri kama Pomonda Raha Beach inayomilikiwa na Rasta Joseph Ndomondo, nimependa ujumbe  wake naamini wanyasa na waingereza wanaelewa kilichozongumzwa katika maneno hayo ya Lugha zao.
Usafiri huo ndio maofisa wa RUNECISO waliutumia kurejea toka kwenye Mdahalo wa wazi wa mabadiliko ya Hali ya Hewa na Mabadiliko ya Tabia nchi wilaya ya Nyasa Jimbo la Mbinga Magharibi ambako tayari wananchi wa Mwambao wanawanyoshea vidole wananchi wa milimani (Milima ya Livingstone) kwa uharibifu wanaoufanya wa kukata miti na kuathiri upatikanaji wa mvua, mtiririko wa maji katika mito inayoingia ziwa Nyasa na kuathiri maeneo ya mazalia ya samaki, mamba na kuharibu mfumo mzima wa uzalishaji wa chakula.

Land-Rovers ndiyo magari madogo yanayoaminikasana huko Mbinga na Wilaya Mpya ya Nyasa kutokana na milima mingi na njia mbaya nyakati hasa za masika.
 
 

Bw Moses Konala Katibu nMsaidizi wa Ruvuma Press Club, akitafakari jambo kuhusu usafiri wa majini, baada ya kuiona Meli ya MV Songea katika Bandari ya Mbambabay ikitokea Kyela Tanzania kuelekea Nkata bay- Malawi wiki hii. Hiyo ilikuwa moja ya shughuli za RUNECISO kufanya Mdahalo wa wazi wa mabadiliko ya hali ya hewa na Tabia nchi yanavyoweza kuathiri maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa Jimbo la Mbinga Magharibi kwa Ufadhili wa The Foundation for Civil Society ya Dar es Salaam.
 
Hapo Makamu Mwenyekiti wa RUNECISO, Bw. Adam Nindi (aliyevaa suti) na Moses Konala wakipanda Bus la SADI kuelekea Liuli. Hapo walikuwepo eneo la Mbambabay baada ya kutembelea bandari hiyo na kuikuta Meli ya MV Songea ikitoka Kyela kuelekea Malawi. Safari kama Kawaida.
 

 
Mtumbwi ziwani Nyasa,  ni chombo cha usafiri na kuvulia samaki.

No comments:

Post a Comment