Pages

Saturday, June 1, 2013

IGP SAID MWEMA AWAVISHA VYEO WALIOULA POLISI NCHINI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema akimvisha cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polis, Thobias Andengenye ambaye hapo awali alikua Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wawili kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na maofisa kumi na tisa kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kuwa Naibu Kamishna wa Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi al Polisi


Na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema amewavisha vyeo maofisa  waandamizi wa  Jeshi la Polisi 21  katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi  jijini Dar es salaam. IGP Mwema aliwavisha maofisa hao vyeo hivyo  baada ya kupandishwa na mheshimiwa Rais  na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi  na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuanzia mei 28 mwaka huu.
 
 Katika hafla hiyo,  IGP Mwema aliwavisha maofisa wawili cheo cha Kamishina wa Polisi  ambao walipandishwa  kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) na kuwa kamishina wa Polisi(CP), maofisa hao ni aliyekuwa Naibu kamishina wa Polisi Suleimani kova  na Naibu Kamishina wa Polisi Issaya Mngulu ambao sasa hivi wamepanda na kuwa makamishina  wa Polisi.
 
Wengine 19,  walivishwa vyeo vya Naibu Kamishina wa Polisi  ambao nao pia walipandishwa kutoka cheo cha kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi na kuwa Naibu kamishina wa Polisi ni Pamoja na Mkuu wa utawala na rasilimali Naibu kamishina wa Polisi(DCP) Thobias Andengenye, Mkuu wa Opereheni Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Simon Sirro, DCP Brown Lekey, DCP Hamdani Omari Makame, DCP Kenneth Kasseke, DCP Sospeter Kondela, DCP Ernest Mangu, DCP Abdulrahman  Kaniki, DCP Adrian Magayane, DCP Husseni Laisseri,  na DCP Anthon Mwami.
 
Wengine kati yao ni DCP Mohamed Mpinga, DCP Mpinga Michael Gyumi, DCP Ally Mlege, DCP Hezron Gyimbi , DCP Jonas Mugendi na DCP Michael Kamuhanda ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa.
 
Miongoni mwa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi  walipandishwa cheo cha Naibu kamishina wa Polisi, wapo maofisa wawili(2) wa kike ambao ni alikuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Bi. Adolfina Chialo ambaye sasa amepanda na kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) na aliyekuwa Kamishina Msaidizi  Mwandamizi wa Polisi Bi. Elice Mapunda naye pia amepanda na kuwa Naibu Kamishina wa Polisi(DCP).
 
Kwa upande wake Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Elice Mapunda alisema kuwa yeye ameshukuru sana kupata cheo hicho, kwani  ni mara ya kwanza  kwa mofisa wa kike wa Jeshi la Polisi  kupata cheo hicho katika  Jeshi la Polisi
 
IGP Mwema alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa rais na amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kutambua mchango wa  utendaji wa maofisa wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao,
 
Aliongeza kuwa “ Ni heshima kubwa sana kwa Jeshi la Polisi   kusema kuwa  amelijengea Jeshi mpanuko mkubwa kwani tangu tupate uhuru mwaka 1961 hatujawahi kupanua jeshi kwa kiwango hiki.
 
 Aliwataka maofisa  walipandishwa vyeo kuwa kioo  na mfano katika kusimamia, kupanga na kutathimini   kwa kuonyesha dira ili maofisa na askari wengine waweze kuiga katika kutoa huduma bora kwa ndani na nje.




Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema akimvisha cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Alice Mapunda ambaye hapo awali alikua Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wawili kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na maofisa kumi na tisa kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kuwa Naibu Kamishna wa Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi al Polisi
 
(SHEREHE HIYO IMEFANYIKA  30/5/2013)
 
via/ lukwangule blog

No comments:

Post a Comment