Pages

Sunday, May 12, 2013

WANANCHI WA WILAYA MPYA YA NYASA MPO? SOMENI HAPA

MBUNGE WA JIMBO LA MBINGA MAGHARIBI, JOHN KOMBA ALIPOKUTANA NA WADAU WA WILAYA YA NYASA.
Na Mwandishi Wetu, Dar

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi ambako sasa imeanzishwa wilaya mpya, alifanya mkutano na wadau wa wilaya Nyasa hapa jijini Dar es salaam. John Komba akiwa  ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Ernest Kahindi na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo walizungumza na wadau wa wilaya Nyasa walioko jijini Dar es Salaam kwa kunia ya kuchochea maendeleo zaidi katika wilaya hiyo. 

Mbunge John Komba akihutubia wadau wa Nyasa, jijini Dar.
Moja ya changamoto kubwa zilizojitokeza ni hali ya matokeo mabaya ya kidato cha nne ambako wilaya Nyasa ilikishika mkia kati ya wilaya zote za mkoa wa Ruvuma. Kwa Mujibu wa mkurugenzi wa wilaya hiyo alisema kunahitajika mchango wa haraka kutoka kwa wadau wa wilaya ya Nyasa ili waweze kufanikisha upatikanaji wa maendeleo. 
Hata hivyo mbunge John Komba aliwaomba wadau hao kuwa ni lazima washiriki kuchochea maendeleo ya wilaya Nyasa tofauti na ilivyo sasa ambako mchango wao ni finyu. Aidha, alihimiza kuwekeza kwa dhati kwa elimu ya watoto wa kike ambapo alisema kwa wilaya ya Nyasa kiwango cha watoto wa kike kusomeshwa ni cha chini sana hivyo aliwaomba wadau kufanya juhudi kubwa kufanikisha ajenda za wilaya zinafanyiwa kazi ipasavyo. 

wadau wa nyasa
Kwa upande wa wadau hao walidai kuwa ni vyema mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa wilaya hiyo wakahakikisha upatikanaji wa vyuo vya ufundi ambavyo vitasaidia vijana wengi wa wilaya hiyo ambao hutegemea kilimo na uvuvi. Pia walisema ni vyema halmashauri ya wilaya ikashirikiana na asasi za dini au AZAKI kufanikisha mpango wa kuanzisha chuo cha uvuvi kama ilivyokuwa Chuo cha Mbegani, kilichokuwa mjini Liuli na kuendeshwa na kanisa la Anglikana. 
Wadau hao walisema halmashauri ya wilaya ihakikishe kunakuwepo vyuo vya mafunzo ya ufundi kwa kushirikiana na VETA ambayo itawakomboa vijana wengi ambao hushindwa kumudu maisha hasa wanapomaliza shule za msingi. mbunge kOmba alisisitiza kuwa ofisi ya mbunge imefanya uchunguzi na kubaini watoto wa kike wengi huishia darasa la saba na baada ya hapo hawasomeshwi, kwahiyo aliwataka wadau kusaidia kuondokana na tatizo hilo ili kuleta uasawa kijamii. 

Nilikuwa miongoni mwao. (Bloger wa Karibuni Nyasa)
Pamoja na mambo mengine makubaliano ya wadau na viongozi wao ilikuwa ni kuboresha elimu, kuvumbua njia mbadala za kuwawezesha wakazi wa wilaya ya Nyasa kuishi katika maisha yenye uhakika kwa kuzingatia elimu ya ufundi. Pia suala la afya lilizingatiwa pia hasa kuboresha hopsitali/zahanati zote za wilaya Nyasa ili kuhakikisha wananchi wanakuwa kwenye hali nzuri. 
Aidha jambo kubwa zaidi ni namna wajawazito wanavyocheleweshwa kufikishwa hospitali kutokana na matatizo mbalimbali. Hata hivyo wadau hao walipongeza juhudi za miradi mbalimbali ikiwemo Maji na ujenzi wa barabara, ambapo kwa sasa upo kwenye upembuzi yakinifu kati ya Mbamba Bay hadi Lituhi, baada ya ujenzi wa barabara ya Songea hadi Mbamba Bay kuendelea kujengwa.
Kutokana na hali hiyo wadau walimhimiza mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mbunge kuhakikisha wananchi wa wilaya Nyasa wananufaika na rasilimali zao zote wilayani humo. Moja ya changamoto kubwa iliyojitokeza ni namna gani serikali itafanya juhudi kuendeleza miradi ya ujenzi wa viwanda mfano Sukari, na vingine. Pia upatikanaji wa soko la uhakika kwa wakulima ambao watakuwa wanauza mazao yao hasa mpunga,mahindi na kadhalika.
wadau
Mbunge, Komba pia alifanya jambo zuri kumwalika aliyekuwa mpinzani wake Alex Shauri ambaye alimhimiza mbunge huyo kuhakikisha kabla ya mwaka 2015 angalau kuwepo na utaratibu wa upatikanaji wa nishati ya umeme. Alex Shauri alisema wananchi wa Nyasa wanahitaji mambo makuu mawili elimu na afya. Akaongeza kuwa kama hayo yatafanyika basi hakuna shaka yoyote kuwa maendeleo ya wilaya yatapatikana watu wakiwa na afya njema, hivyo upatikanaji wa madawa na matibabu yenye uhakika ni muhimu zaidi.
wadau
Kwa upande mwingine wadau walikubaliana na mbunge kuwa changamoto ya mchango wao kuwa finyu itafanyiwa mabadiliko, ambapo hapohapo kulianzishwa harambee ya kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo. 
MUHIMU; picha za wadau wa Nyasa waliohudhuria mkutano huo katika ukumbi wa Msimbazi Center wa kanisa katoliki jijini dar es salaam.

sehemu ya waliohudhuria.

wadau
 
Source: Karibu Nyasa Blog.

No comments:

Post a Comment