Pages

Monday, May 13, 2013

MWENDESHA PIKIPIKI (YEBOYEBO) AGONGWA NA BUS ASUBUHI HII


Waendesha Pikipiki wakiwa wameinyanyua Pikipiki ya mwenzao aliyegongwa na Bus Asubuhi mwendo wa Saa 2:45  hivi eneo la Moonlight  Bombambili karibu na Ofisi za TBC Kituo cha Kanda ya Ziwa Nyasa Songea, kwenye matuta  karibu na Jengo la Mzee Songambele . Aliyegongwa alikuwa amekimbizwa Hospitali na Kufahamika kwa jina Moja tu la Kurwa Mjuukuu wa Mzee Mustafa mangolingoli wa Making'inda Msamala Songea.

Wasamalia wema wakiikokota Pikipiki iliyopata ajali  pembezoni mwa barabara ya Songea - Makambako hapa Manispaa ya Songea



Watu wakiendelea kushangaa ajali hiyo asubuhi hii eneo hilo hilo hapo Moonlight Bombambili  Songea, kabla ya kutokea kwa Askari wa Usalama Barbarani.  Walioshuhudia ajali hiyo wanasema Bus ndio limemgonga kijana  Kurwa na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa Songea, (Homso). (Picha na Maelezo na Juma Nyumayo)


No comments:

Post a Comment