Pages

Monday, May 20, 2013

WANAKIJIJI WAFURAHIA KUONA UMEME KWA MARA YA KWANZA TOKA KUUMBWA KWA DUNIA

Vifaa vya Umeme Jua


Na Steven Augustino, Tunduru

WAKAZI wa Kijiji cha Tinginya, tarafa ya Nakapanya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wamelipuka kwa furaha baada ya kupata umeme kwa mara ya kwanza tangu dunia iumbwe kijini kwao.
Kwa namna ya pekee wakazi hao, wameipongeza Serikali kwa kuwafungia Mfumo wa Umeme Jua (SOLA) katika Zahanati yao na kueleza kuwa mradi huo utawakomboa wanawake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakijifungua wakiwa gizani.

Kwa nyakati tofauti, wakazi hao wakiongozwa na Fatuma Mapila na Bw. Aliahad Abdalahman ambao walikuwa wamepeleka mtoto wao kwa ajili ya matibabu na Muuguzi wa Zahanati hiyo, Grolia Lupindo ni miongoni mwa baadhi ya wananchi ambao walishindwa kuzuia furaha yao baada ya kushuhudia wakati mfumo huo ukiwashwa katika zahanati yao na katika nyumba ya Mganga wa zahanati hiyo.

Wakifafanua taarifa hiyo walisema kuwa  kwa muda mrefu tangu Zahanati yao ifunguliwe mwaka 1990 hadi siku hiyo wanawake wa Kijiji hicho na vitongoji jirani walikuwa wakitumi vijinga vya moto kumulikia wakati wa kujifungua ama kujifungua katika giza hali ambayo ilikuwa ikihatarisha maisha yao na watoto wanao jifungua.

 Awali akiongea na wananchi hao afisa mafunzo na ujengaji wa uwezo kutoka wakala wa nishati Vijijini (REA) Mary Ngusaru alisema kuwa ufungaji wa mfumo uliofanywa na kundi la vijana 35 walio maliza mafunzo ya siku 7 na kwamba hivi sasa Wilaya ya tunduru imepata hazina ya mafundi wengi wenye uwezo wa kufunga na kufanya matengenezo madogomdogo ya mfumo huo wa meme jua.

Bi.Ngusaru aliendelea kufafanua kuwa hadi kuamilika kufungwa kwa mfumo huo na mfumo mwingine utakaofungwa katika Zahanati ya kijiji cha Nampungu  utaghalimu jumla ya shilingi Milioni 20 ambazo zimegahilimiwa na serikali kupitia mpango wa changamoto za milenia (MCC) na kwamba serikali inaamini kuwa miradi hiyo itatunzwa na kusaidia kupunguza uhalibifu wa misitu kwa ajili ya matumizi ya nishati ya kuni.

Nae Mwezeshaji wa mafunzo hayo  Mhandisi  Philbert Beyanga, kutoa kampuni ya Solar Energy alisema kuwa katika kipindi hicho  vijana hao  watanolewa  na kupatiwa ujuzi  na uendelezaji wa teknolojia za umeme jua,nishati upepo,nishati tungamotaka na nishati ya moromoko madogo ya maji.

Alisema mfumo huo unao uwezo wa kuwasha taa 36 pamoja na  kumudu kuendesha mashine za kupimia malaria hali ambayo itawarahisishia kazi watumishi wa zahanati hiyo.

No comments:

Post a Comment