Pages

Tuesday, May 21, 2013

WANAFUNZI WA SHULE ZA AWALI WATESWA NA MADAWATI



"Shikamooooooo!!! Mwaaaaalimu," Wanafunzi wa darasa la awali Bombambili Manispaa ya Songea wakiamkia Asubuhi ya leo, shida kubwa wanayokabiliana nayo wanafunzi hao wapatao 41 ni madawati wanayokalia ni makubwa kupita umri wao na kuwafanya washindwe kufuatilia masomo kwa vitendo hasa kuandika. (Picha na Juma Nyumayo)

Vibao vya Kuonyesha Shule zilipo, ni Muhimu sana katika maendeleo ya Shule za Msingi . Vibao hivyo ni vya Shule za Msingi Bombambili na Shule ya Msingi Mputa iliyotokana na S/M Bombambili kuwa na wanafunzi wengi.

Saluti kwa saaana.



Wavulana wakitoa heshima yao kwa kuamkia darasani mwao. Mafunzo ya awali ni muhimu sana katika kuwajenga wanafunzi utayari wa kupokea masomo ya Shule ya Msingi.


Wanafunzi wa awali wakiwa wamekalia madawati ya kaka na dada zao wa Shule ya Msingi. Madawati hayo ni makubwa kupita umri  na maumbo yao.


Mwalimu Benedetha Kilapilo, wa Shule ya Msingi Bombambili Manispaa ya Songea akimsaidia Mwanafunzi wa Darasa la Awali leo, Shuleni hapo (Picha na Juma Nyumayo)




No comments:

Post a Comment