Pages

Wednesday, May 22, 2013

KAKAKUONA SONGEA, ALETA VITUKOUSIKU WA KUAMKIA VURUGU ZA MTWARA , ACHAGUA MKUKI SHOKA NA UPANGA


Kakakuona siye wa tukio halisi)
Na Juma Nyumayo, Songea

MNYAMA Mwenye heshima kubwa miaka dahari na dahari katika makabila na mila mbalimbali za kiafrika, Kakakuona ambaye huonekana kwa nadra sana, amejitokeza tena hapa Songea na kuleta vituko vya kukata na shoka usiku wa kuamkia siku ya vurugu za watu wa Mtwara kupinga kujengwa kwa bomba la kusafirisha gesi asilia toka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Kakakuona huyo alionekana na kukamatwa na watu wa eneo la Lipupuma Mtaa wa Mshangano, Manispaa ya Songea juzi usiku mishale  ya saa 4 hivi na kuwalazimu kuwatafuta viongozi wa serikali na mila hasa wazee.
Vizazi vya makabila mengi hapa Tanzania, ikiwepo mimi nayeandika habari hii vimeaminishwa kuwa apatikanapo Kakakuona lazima achezewe ngoma, au apelekewe vifaa mbalimbali watumiavyo watu hao ikiwa ni pamoja na vile vya kivita, mbegu, na maji ili kutabiri neema au majanga kwa jamii aliyoenekana.
Mzee Vitus Mtazama Mbano (87) wa pili toka kushoto
Hapa Songea, usiku huohuo walimjulisha Mwenyekiti wa Mtaa wa Mshangano, Paul Mangwe, na wazee wa kingoni akiwapo mjukuu wa Ukoo wa Chief Songea Mbano, Mzee Vitus Zimanimoto Mbano (86) wa Mshangano ambaye aliongoza jukumu la kusema maneno ili kakakuona huyo afanye utabiri wake.

Kakakuona huyo mishale ya saa 7.00 usiku wa kuamkia jana akakacha maji, unga, mbegu za mahindi, mpunga, mihogo, na nafaka mbalimbali alizowekewa na bahati mbaya au kwa mazoea au kusahau hawakukumbuka kumwekea simu za mkono, Computer ili atabiri mafaniko ya maendeleo ya sayansi na teknolojia iliyofikiwa sasa.
Bila ajizi akaviendea vitu vya hatari vinavyoashiria vurugu na vita. Si vinginevyo vilivyokuwepo hapo ni panga, Mkuki na Shoka.
Haikuwa rahisi kwa kakakuona huyo kuchukua hatua hiyo baada ya kuanza sherehe yake hiyo kwa kusindikizwa na maneno ya kijadi kwa kabila la kingoni akiongoza Mzee Mbano aliyezaliwa mwaka 1927 kuanzia mishale ya saa 4. hivi usiku hadi saa 7 kuamkia siku ya vurugu za watu wa Mtwara wanaopinga kujengwa kwa Bomba la Gesi asilia toka Mtwara hadi Dar kwa matumizi ya kuzalisha nguvu za umeme na matumizi mengine ya viwanda.
Akizungumzia mikwala ya Kakakuona huyo, ambaye tayari amekabidhiwa Ofisi ya Maliasili na kuchukuliwa na maafisa wanayamapori mjini hapa, Bw. Samwel Mbano mkazi na mmiliki wa eneo ilipofanyika shughuli hiyo, alisema usiku wa saa tisa kakakuona huyo alipandishwa katika gari na hakutaka kushushwa tena kwa kung'ang'ania 'Rim' la gurudumu la Motokaa  lililowekwa katika "Buti" ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mshangano Bw.Paul Mangwe ambao waliamua kazi hiyo ya kumshusha ifanyike jana (asubuhi tarehe 22/5/2013) ambapo tulipokea taarifa za vurugu mbaya kabisa huko Mtwara zilizosababisha hasara kubwa ya mali na kupotea kwa uhai kwa raia mmoja, wanajeshi wanne wa kambi  ya Nachingwea kufa katika ajali wakiwahi kutuliza vurugu hizo.
Hasra nyingine ni pamoja na kusitishwa kwa safari za ndani mkoani humo, kuchomwa kwa majengo ya ofisi na nyumba za raia ikiwamo ya Mwaqndishi wa habari waTBC1 Kassim Mikongolo na kuharibu miundombinu mbalimbali.
Mwisho

No comments:

Post a Comment