Pages

Thursday, May 23, 2013

POLISI RUVUMA WAKAMATA TENA PEMBE ZA NDOVU

Kamanda Nsimeki akionyesha Pembe za Tembo leo
Na Juma Nyumayo, Songea
JESHI la Polisi kwa mara nyingine tena Mwezi huu limekamata Pembe za Tembo zenye thamani ya shilingi milioni 8,398,000 kutoka mtandao wa majangili wa Kijiji cha Mandepwende  wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.
Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, amemuambia mwandishi wa habari hizi  nje ya Ofisi yake kuwa  yeye na Kikosi cha kuzuia Ujangili Kanda ya kusini wamejipanga vizuri na ndio maana Mtandao wa Majangili umebanwa kila kona.
"Nakuambia hawa tutawabana kila kona, maana nakili kuwa tunafanya kazi kwa uelewano mkubwa na kikosi cha Kuzuia ujangili kanda ya kusini," alisema Kamanda Nsimeki akitamba kuwa sasa ndio Arobaini yao.
Alisema ametoa wito kwa wanchi wema kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama na pia kuwatahadharisha wote wanaojihusisha na biashara hiyo waache mara moja.
Pembe za ndovu zilizokamatwa ni 11 ambazo ni sawa na Tembo sita ambao wameuawa na majangili hao.
Hivi karibuni, jumuia za kimataifa zimelaani biashara ya pembe za tembo ambazo zimesababisha kuuawa kwa Tembo wengi hapa Afrika. Miongoni mwa mataifa yanayolaumiwa zaidi ni pamoja na nchi za Afrika Mashariki Tanzania ikiwa mojawapo.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki akiwaonyesha waandsi wa Habari (Hawapo pichani) Pembe mbili za ndovu miongoni mwa zilizokamatwa zenye Thamani ya  Shilingi milioni 8,893,000. Pembe hizo zote zimekamatwa Kijiji cha Mandepwende  wilayani Namtumbo.
 
Naye  Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kusini  Abedi Mwari, (Mwenye shati la kiraia) akimuonyesha hesabu kamili ya Pembe zilizopatikan Kamanda Nsimeki (Mwenye Sare ya Polisi) huku waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo  katika Ofisi ya Polisi Mkoa wa Ruvuma leo

No comments:

Post a Comment