Pages

Thursday, May 23, 2013

NINI HATMA YA USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI --- BARUA

Waandishi wa Habri wakiwa kazini .
Barua toka Songea.
Ni Barua inayokwenda kwa wananchi, viongozi na wanahabari waandishi wote Tanzania
Ni Barua inayohitaji majibu kwa maneno na vitendo.
Tiririka,

Ndugu zangu naandika ujumbe huu nikiwa na hudhuni kubwa. Mzee kassim Mikongolo wa TBC1 Mtwara amechomewa nyumba yake na gari lake vyote vimeteketea. Hii inamaana hata yeye wangeweza kumuangamiza kabisa. Mzee huyu ni mwandishi wa habari anayetegemea kustaafu kazi zake. malipo kwa watu wake anaowatumikia ni kuteketeza kila kitu chake kwa moto.

Kisa eti yeye ni Mwandishi wa habari anayefanyia kazi katika chombo cha serikali (huenda sina ukhakika). Hiyo ya kufanyia chombo cha serikali hata Martina Ngulumbi wa TBC1,  Lindi alilalamika kupitia kipindi cha Jungu Kuu-Usiku wa tarehe 22/5/2013 kwamba alipata ujumbe wa simu -sms-wa mtindo huo kwamba watakiona.

Leo, tunashuhudia nhatari hii. Kesho yatatupata mambo gani waandishi . hatutakiwi kabisa kushabikia vurugu, maana vurugu zikianza hakuna Mwandishi atakayekuwa salama. Kwa maneno yake mwenyewe kassim Mikongolo alisema alipiga bsimu polisi kwa msaada kuzuia wahalifu hao. polisi walimjibu wapo mikindani kunavurugu kubwa zaidi huko. Na walivyofika hapo walikuta majivu tu.
Imeniuma sana na hasa ninavyotafakari muafaka na mstakabali wa waandishi wa habari hapaTanzania ambao wengi wao ni wanajitolea zaidi kuliko ujira waupatao.
Ni wazi kuwa wananchi wa nchi hii sasa uamuzi wao na chuki zao zinazo elekezwa mara moja kwa waandishi wa habari waliokaribu na matukio kwa kudhani wao ndio wakala wa kundi Fulani, ni hatari nyingine kuliko tunavyofikiri.
Naomba maoni yenu tufanye nini kabla hatujamalizwa.
Hapa ninamaana ya kumalizwa kinchi kwani nchi bila habari si nchi tena. "taarifa ni nguvu" .
Kuna makongamano, midahalo maombi  na mbinu mbalimbali kuhusu usalama wa waandishi wa habari ya kutaka walindwe hazijafua dafu.
Majibu ya miaka nenda rudi ni kwamba tunawalinda waaandishi  kama raia wengine lakini mmoja mmoja anaondoka kama swala au pundamilia katika pori la Simba.
Je ni kweli wanasiasa ni chanzo cha vurugu na kuteswa kwa waandishi wa habari? au ndo kusema njaa za waandishi kama wanaobeza? au raia hawana uelewa wa kutosha kujua umuhimu wa wandishi, jambo ambalo mimi napinga. Kazi hii ni kutekeleza Wajibu kama wanavotekeleza wengine. Naomba majibu.


Wasalaaam
Wenu anayesubiri majibu
Juma Nyumayo
Manispaa ya Songea

No comments:

Post a Comment