Pages

Wednesday, April 17, 2013

BW. GERSON MSIGWA WA TBC-SONGEA APATWA NA MSIBA

Bw Gerson Msigwa, ( kulia ) akiangalia utaratibu wa msafara wa magari kuelekea Iringa kwenye Mazishi ya Msiba wa dada yake wakati wasindikizaji wakipanda gari lililochukua Mwili wa Marehemu.
Mmoja wa Ndugu akitoa shukurani ya michango ya rambirambi na kuwasoma watakao safari kwenda mazikoni Iringa jioni hii.

Ndugu jamaa na Marafiki wakibeba Sanduku la Mwili wa Marehemu toka ndani ya nyumba yao,  tayari kuingiza kwenye Bus la Super Feo kwa safari ya Iringa wakitokea  eneo la  Mfaranyaki, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma jioni hii.

Sanduku la Marehemu likiingizwa ndani ya Bus la Super Feo tayari kwa maombi na Safari ya kwenda  Iringa kwa mazishi.

Sanduku la Mwili wa marehemu laingizwa katika Bus



Maombi ya Safari ya kwenda Iringa kwa Mazishi yakiendelea na badhi ya ndugu na jamaa wakishiriki.

Mzee Thomas Lipuka Komba (Kushoto) na Nathan Mtega ni miongoni mwa Waandishi wa habari  waliohudhuria kuaga mwili wa Marehemu hapo Mfaranyaki Songea Manispaa leo jioni.
Mungu alitoa, Mungu ametwa. Tunawaombea safari njema na maziko mema
(Picha Zote na Juma Nyumayo)


No comments:

Post a Comment