Pages

Tuesday, April 30, 2013

GONGO YAMPELEKA KUZIMU MWALIMU MSTAAFU



Mtambo wa Pombe ya Moshi maarufu kama 'Gongo'


Na Steven Chindiye, Tunduru
MWALIMU mstaafu katika Kijiji cha Kidodoma Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma, Rajab Mohamed, Kalesi (65) amefariki dunia baada ya kunywa pombe haramu ya Moshi ambayo inafahamika kwa jina la Gongo.
Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mdogo wa marehemu Athuman Saidi, walisema kuwa kabla ya mkasa huo marehemu alionekana akinywa Pombe hizo kwa siku mbili mfululizo akiwa amefungiwa katika nyumba ya muuzaji wa pombe hiyo Hamdi Swalehe huku akiwa anatamba kuwa ana fedha nyingi alizokuwa ametoka kulipwa kama mafao ya kustaafu kazi hiyo.
Walisema kufuatia taarifa hiyo ya kupokea fedha hizo zinazo daiwa kuwa zilikuwa ni zaidi ya Shilingi Milioni 48 mstaafu huyo alionekana kutembea na wapambe muda wote huku wakienda kujipatia kinywaji hicho kwa wingi na kumsababishia dhahama hiyo ya kupatwa na umaiti.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Diwani wa viti maalumu wa Tarafa ya Nampungu Rehema Nyoni na Mtendaji wa Kijiji hicho Mbuyu Ally Mbuyu walisema kuwa baada ya wapambe hao kuona hali ya tajiri yao imebadilika walitimua mbio na kumtelekeza katika nyumba ya muuza pombe hiyo hadi umauti ukamkuta akiwa peke yake.


Walisema akiwa katika hali yha kutapatapa Mke wa muuza pombe hiyo alijitahidi kuokoa maisha yake kwa kumpatia huduma ya kwanza kwa kumpepea, kummwagia maji ya baridi na baadae akamnywesha uji lakini hali ilizidi kuwa tete na alipo kata roho mumewe Hasani Swalehe alitimua mbio na kumwacha marehemu akiwa juani.


Akizungumzia tukio hilo Mganga aliye ufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Kalesi Dkt, George Chiwangu alisema kuwa chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na unywaji wa pombe nyingi.


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kufuatia hali hiyo wanamshikilia mke wa muuza pombe huyo ambaye hakumtaja jina lake kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

UTAMU WA KUSOMA HUU HAPA


Mhariri wa Gazeti la Tujifunze, Kanda ya Kusini, Bw. Christian Sikapundwa, akisoma Kitabu cha Mwandishi Nguli wa Kiswahili Afrika Mashariki, Shaaban Robert, "Maisha yangu na Baada ya Miaka Hamsini" Usomaji vitabu ni jambo la maana sana kwa wanataaluma uandishi wa habari. (Picha na Juma Nyumayo)



Naomba usome kwa makini Beti  hizi mbili za  Utenzi wa Adili   toka Uk. 24 kitabu hicho hapo juu cha  Shaaban Robert
 
kisha tafakari....(Juma Nyumayo)
 
20. Amemiliki elimu,
      Kila kitu afahamu,
      Kwake hapana gumu,
      Asilojua mbinuye.
 
21. Yeye ni mfafanuzi,
      Dunia kwake i wazi,
      Wala hakuna tatizi,
      Itatizayo kaziye.
 
 
 
 
 
     
 


Monday, April 29, 2013

WAFUGAJI KUKU WACHANGAMKIA VIFARANGA SONGEA


Wateja wa Vifaranga Manispaa ya Songea, wakisubiri zamu ya kupokea vifaranga wakiwa wamekaa kwenye  Bench, na wengine wakiwa wanaondoka na vifaranga wao kwenye maboksi toka Ofisi ya Euro Poutry iliyopo Jengo la CCM Tawi la Mjini, Mtaa wa Zanzibar, Manispaa ya Songea. Wafugaji wa kuku wanaendelea kuongezeka mkoani hapa kutokana na mahitaji makubwa ya nyama na mayai pia uelewa wa ujasiliamali miongoni mwa wakazi wa Manispaa ya Songea, hasa wanawake. (Picha zote na Juma Nyumayo)



W

Boksi la Vifaranga 100 ambavyo huuzwa kwa Tsh. 160,000 @ Tsh 1,600/= tu.


Wateja wakiondoka na vifaranga tayari kwa kufuga

WAZEE WASTAAFU WALIA NJAA RUVUMA



Baadhi ya Wazee wakielekea NMB Tawi la Matogoro, Songea wengine pale mbele kushoto karibu na Mashine za ATM nje wakiwa wamekaa chini wsijue la kufanya baada ya kukosa fedha zao za Pensheni. (Picha na Juma Nyumayo)










Mzee Mstaafu Bw. Holela maarufu kama Mkandamkanda (Kulia) akimsimulia kadhia ya kukosa Pensheni Mhariri waTujifunze  Kanda ya kusini, Bw. Christian Sikapundwa (Kushoto) yeye ni miongoni mwa wastaafu wanaolia  njaa Mkoani Ruvuma 

Baadhi ya Wazee wastaafu wakikatisha mtaa kuelekea Benki ya NMB Tawi la Matogoro, Songea upande wa kushoto leo kuangalia kama Pensheni yao imetoka. (Picha na Juma Nyumayo)






 
 









NA Juma Nyumayo, Songea.

KATIKA hali ya kutia simanzi na masikitiko makubwa, wazee wastaafu wa serikali mkoani Ruvuma, wanaendelea kulia njaa baada ya kukosa fedha zao za Pensheni wiki hii.

Wazee hao wanaotoka karibu kila kona za mkoa huu, wakisafiri umbali mrefu  kwa nauli za kukopa na hata wale wanaotembea kwa miguu wameambulia patupu.

Wakizungumza na mtandao huu, kwa nyakati tofauti karibu na Tawi la Benki ya NMB, Manispaa ya Songea leo,  wamesema hivi sasa wanakabiliwa na matatizo makubwa kwa wale waliowakopa na changamoto ya kujikimu hapa mjini na familia walizoziacha huko walikotoka.

" Hali yetu ngumu sana kifedha, kama ujuavyo sisi ni wazee hutegemea Pensheni kila baada ya miezi mitatu, huu ni karibu  mwezi wa nne, hakuna kitu," alilalamika Mzee Mstaafu ajulikanae kwa jina moja tu la Mapunda toka Wilaya mpya ya Nyasa.
Mzee mapunda anasema alikuja Songea toka Aprili 25 mwaka huu kufuata Pensheni yake akiwa na bajeti ya Nauli, Madeni kibao yenye riba toka huko Mbambabay - Nyasa.

Mzee Mwingine ni aliyekuwa mtumishi wa Idara ya Kilimo, Driver maarufu  Manispaa ya Songea, kwa Jina la Mkandamkanda, ambaye yeye amepaza sauti kuwa hivi sasa hajui mkewe amjibu nini maana hawana kitu na hategemei kukopeshwa.

"Sielewi mke wangu ni mjibu nini! maana hamna kitu," alilalamika Mzee mkandamkanda aliyestaafu kazi mwaka 2007.
Wazee hawa ambao walilijenga taifa hili kwa nguvu moja baadhi yao walikwenda kuulizia Hazina Ndogo Ruvuma kama serikali imetoa pesa yao. Wengi wao wameelezwa kuwa serikali imetoa pesa na kupelekwa NMB Tawi la Songea tayari kwa malipo.
" Tumejibiwa pesa zimepelekwa NMB, na NMB tukiangalia salio hamna pesa," alisema Mkandamkanda.

"hapa sisi tunapigwa danadana kama mpira, hali zetu ngumu na amini kila mzee ni mgonjwa kwa kukosa nguvu za kifedha na afya," alisema Mkandamkanda kwa hisia kubwa.
Tatizo la kucheleweshewa Pensheni wazee linawakosesha raha si wao tu bali hata waajiriwa waliopo kazini kwani ni wazee wastaafu watarajiwa.

Wazee hao kwa niaba ya wenzao wameliomba Bunge linaloendelea Dodoma na wizara husika kuhakikisha wanapewa Fedha zao mapema ili waweze kujikimu kimaisha.

Uchunguzi wa Blogu hii umeoneshwa wastaafu kukatishwa tama na hatua za polepole zinazochukuliwa kushughulikia fedha hizo za Pensheni na kuwafanya baadhi yao wajutie utumishi uliotukuka walipokuwa waajiriwa.
Mwisho

 


Sunday, April 28, 2013

MKUTANO WA MARAFIKI WA ELIMU SONGEA


WASHIRIKI WA MKUTANO WA MARAFIKI WA ELIMU SONGEA WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAELEZO  YA MWEZESHAJI (HAYUPO PICHANI) KABLA YA UFUNGUZI


MWENYEKITI WA MKUTANO HUO, BW. LAURENT MBEWE (MEZANI JUU) AKIFUATILIA RATIBA INAYOSOMWA NA MTUNZA MUDA MWL. MPENDWA MILANZI ALIYESHIKA KARATASI CHINI.


MGENI RASMI, RAFIKI WA ELIMU BW. GORDEN SANGA MAARUFU SANGA ONE( ALIYESIMAMA) AKISISITIZA JAMBO HUKU AKIMUANGALIA BW. NYANDA (KUSHOTO)  MWAKILISHI WA HAKIELIMU  KUTOKA DAR ES SALAAM WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO HUO WA MARAFIKI WA ELIMU SONGEA, KATIKA UKUMBI WA SACCOS YA WALIMU SONGEA VIJIJINI MANISPAA YA SONGEA


MSHIRIKI ALIYEPEWA JUKUMU LA KUFUATILIA HOTUBA YA UFUNGUZI AKIANDIKA VIPENGERE MUHIMU


MGENI RASMI GORDEN SANGA AKIMALIZIA HOTUBA YAKE, HUKU MWANDISHI WA JOGOO FM, TAMIMU ADAM GILLO, AKIREKODI HOTUBA HIYO MUHIMU ILIYOSISITIZA UWAJIBIKAJI KATIKA KUSIMAMIA ELIMU YA WATOTO WETU HAPA SONGEA


MWENYEKITI WA KAMATI YA SHULE YA MSINGI MASHUJAA, MZEE INOCENT NYONI, AKISHUKURU HOTUBA YA MGENI RASMI KWA NIABA YA WASHIRIKI WENGINE

PICHA YA PAMOJA YA WASHIRIKI NA MGENI RASMI, BW. GORDEN SANGA ALIYEKAA KATIKATI MWENYE SUTI NYEUSI


TOKA KUSHOTO ALIYECHUCHUMAA MWL HERI SALUM MATOPE, MTOA MADA NA MTUNZI WA KITABU CHA TANZANIA MIAKA HAMSINI TULIKOTOKA, TULIKO, NA TUNAKOKWENDA, FR. JOHN MTWALE KASEMBO, KUTOKA SEMINARI KUU PERAMIHO, BW. SWAI TOKA HAKIELIMU, DAR, MGENI RASMI SANGA ONE, MZEE LAURENT MBEWE, AFISA ELIMU EWW, FARAJA TOKA  SONGEA MANISPAA NA BI. RUFINA MBUNDA.


PICHA YA PAMOJA KAMA HAPO JUU.  TOKA KULIA ALIYEKAA,  MHESHIMIWA DIWANI WA KATA YA MJINI, BW. FUIME AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI ALIYEFUNGA MKUTANO HUO. 


KAMA HAPO JUU. WALIOONGEZEKA NI STEPHANO MANGO ALIYECHUCHUMAA KUSHOTO NA WALIOKAA KATIKA VITI WA PILI TOKA KUSHOTO NI BW. JUMA NYUMAYO AMBAO WALIANDAA MKUTANO HUO WAKISHIRIKIANA NA MARAFIKI WENGINE WA ELIM U SONGEA

PICHA YA PAMOJA KAMA JUU


AFISAELIMU  WA MANISPAA MWL.FARAJA AKIFAFANUA JAMBO KUHUSU SHULE MBILI ZA MSINGI AMBAZO HAZIJAANZISHA MADARASA YA AWALI KATI YA SHULE ZA MSINGI 76 ZILIZOPO MANISPAA YA SONGEA.
SHULE HIZO ZIMEELEKEZWA KUFUNGUA MADARASA HAYO MAPEMA MWAKANI.

MWANAFUNZI TOKA SHULE YA WALEMAVU WASIOONA LUHIRA, SHAAME, AKIELEZA MATATIZO YANAYOWAKABILI WANAFUNZI WASIIONA WAKATI MWANDISHI WA REDIO JOGOO FM, TAMIMU ADAM AKIREKODI CHANGAMOTO HIZO.


SEKRETARIETI: MWL. HENRY SALUM MATOPE  NA GLORIA AMBAO WAKIENDELEA KUANDIKA CHANGAMOTO ZA MARAFIKI NA MAJIBU YA MAAFISA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI MANISPAA YA SONGEA 


MWAKILISHI WA AFISA ELIMU WA SEKONDARI. MWL. KOMBA AKIELEZEA TAARIFA ZA SEKONDARI KWA WASHIRIKI WA MKUTANO WA MARAFIKI WA ELIMU SONGEA.


BABA FR. JOHN MTWALE KASEMBO  (PICHA YA JUU NA CHINI) AKISISITIZA UMUHIMU NA WAJIBU WA SERIKALI, WAZAZI, WANAFUNZI NA MARAFIKI WA ELIMU KATIKA KUENDELEZA NA KUBORESHA ELIMU YA WATANZANIA KWA MAENDELEO YAO NA ULIMWENGU KWA UJUMLA. 




MARAFIKI WA ELIMU SONGEA WAPATA VIONGOZI WAKE


Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Marafiki wa Elimu Songea (Waliokaa toka kushoto) Makamu Mwenyekiti Mwl. Henry Salum Matope, Mwenyekiti, Juma Nyumayo na Mpendwa Milanzi. (Waliosimama kutoka kushoto) Mratibu wa Marafiki, Stephano Mango, Bw. Nyanda toka hakielimu DSM,  Bw. Zakaria Ndumbaro,  Mzee Laurent Mbewe, Happiness Hinju, Mzee Inocent Nyoni, Bw. Ng'oko, Bi Rufina Mbunda, Bi Gloria Lawrence na Afisa toka Hakielimu DSM, Bw Swai.  


Monday, April 22, 2013

JUMBA LA KIFAHARI LA MCHUNGAJI,. MHE. GETRUDE LWAKATARE KUVUNJWA?

Wabunge walia na hekalu la Mchungaji Lwakatare
NYUMBA YA MCHUNGAJI GETRUDE LWAKATARE, MHESHIMIWA MBUNGE (VITI MAALUM - CCM)
Mchungaji Getrude Lwakatare (MB) Katikati akiw na MC siku ya Ufunguzi wa Jumba lake.

WABUNGE wamemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Terezya Huvisa kuzivunja nyumba mbili zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam zilizojengwa katika fukwe ya bahari ya Hindi ikiwemo ya mbunge licha ya kwamba kuna zuio la Mahakama.

Bila kutaja majina ya wamiliki hao, wabunge hao walitaka hatua hizo zichukuliwe kwa haraka kwa nyumba hizo zilizojengwa kwenye fukwe kinyume cha sheria zivunjwe kwa maelezo kuwa hazina ofa wala hati.

Sambamba na hilo wametaka watendaji wa Serikali waliohusika kutoa vibali kuruhusu ujenzi huo kwa maelezo kuwa walichukua rushwa wachukuliwe hatua.

Mbunge wa kwanza kuanza kuzungumzia hilo ni wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) aliyetaja viwanja viwili vyenye namba 2019 na 2020 kikiwemo cha mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani waliojenga nyumba zivunjwe licha ya kuwepo zuio la Mahakama.

“Mwaka jana Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka alivunja nyumba za kawaida licha ya zuio la Mahakama, lakini nyumba zilizo kwenye viwanja namba 2019 na 2020 hazikuvunjwa kwa sababu ya zuio la Mahakama hii ni double standard (ndumilakuwili) hatuwezi kuvumilia.

“Wengine wenye nyumba ni viongozi tupo nao humu tena wa kiimani, lakini kwa nini viongozi tunafanya hivi wakati tunatakiwa tuwe wa mfano na tunawafanya viongozi wenzetu washindwe kufanya kazi zao?… hakuna haja ya kuogopa Waziri Huvisa (Mazingira) vunja nyumba, haiwezekani kuwa na nguvu ya fedha.

“Wabunge wenzangu tuazimie Manispaa ya Kinondoni na NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira), wakavunje nyumba hizo ndani ya wiki moja , naomba kutoa hoja,” alisema.

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimweleza; “Haiwezekani kutoa hoja kwa kuingilia vyombo vingine”.

Mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani mwenye nyumba katika eneo hilo la Mbezi Beach aliyejenga katika fukwe ya bahari kwa kuondoa mikoko na kuweka kifusi na kujenga nyumba ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Dk Getrude Lwakatare (CCM). Hata hivyo wakati wa michango hiyo mbunge huyo hakuwa ndani ya Bunge.


Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Kiwelu (Chadema) akichangia bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, alisema Kamati yake ya Ardhi na Mazingira ilitembelea eneo hilo la Mbezi Beach na kukuta aliyejenga katika kiwanja 2019 hakuwa na ofa wala hati.

“Ametumia pesa kuwarubuni watendaji akaondoa mikoko, akaweka kifusi na akajenga nyumba naomba Wizara ya Ardhi na ya Mazingira wawachukulie hatua watendaji hao,” alisema.

Akijibu hoja ya Bulaya, kuwa kwanini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuvunjwa wakati nyingine zilivunjwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema alisema: “Sisi ni wajibu wetu twende mahakamani kusema watu hao wamevunja sheria kujenga hapo.

Wao wanaruhusiwa na Katiba na Mahakama itafuata sheria. “Nashauri Bulaya usitoe Shilingi kuzuia Bajeti ya Waziri, uje tuone huyo kigogo itakuwaje.” Hata hivyo, Huvisa alisema: “Nyumba tulizovunja hazikuwa na kesi na hii tuliyoiacha ilikuwa na kesi.”

Jumba la kifahari linalodaiwa kuwa la Mchungaji Lwakatare ambalo lilizinduliwa mwaka jana, limekuwa likitajwa kuwa lina thamani ya takribani Sh bilioni 1.5.

chanzo; HABARILEO 

Saturday, April 20, 2013

JUMA NATURE ATIMULIWA EATV BAADA YA KUINGIA AKIWA AMEVAA KANDAMBILI


Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassim Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kitendo  cha  kutimuliwa  jana usiku katika kipindi cha burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview. 
Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo  mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi  na ndipo Nature hakuonekana tena.
  Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfuata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika yafuatayo  kupitia ukurasa wake wa facebook....



"hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo....

kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview"
SOURCE. freebongo.blogspot.com

PEPO GANI KAINGIA MJENGONI?


JENGO LA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LILILOPO DODOMA.


Na Juma Nyumayo, Songea.
 
MJADALA Mkubwa umeibuka katika nchi ya Tanzania kuhusu kinachoendelea katika Bunge huko Dodoma.
Mjadala huu umechukua sura ya namna yake  kutokana na Matusi ya nguoni, kejeli, dharau na kile kinachotafsiriwa na watu wa makundi mbalimbali kuwa wabunge hao wameacha walichoendea Dodoma.
Hivi sasa, katika ngazi ya familia, mjadala huo umechukua sura ya watoto na wazazi wao au walezi kupeana majina kuwa wasifanye kama waheshimiwa wafanyavyo mjengoni.
 
Kwaujumla, Wabunge wamewaangusha wapiga kura wao. Namaanisha hata wabunge amabao hawajawahi kufunua midomo yao tangu waingie Mjengoni hapo, hawakwepi lawama hii.
Mwanafunzi mmoja aliniuliza nikiwa kama Mwandishi wa habari.
Mwanafunzi: Eti waheshimiwa wabunge walikuwa hawataki Bunge lioneshwe "live" ili watukane?
 
Mimi: Wewe umemsikia nani?
Mwanafunzi: Wanasema baadhi ya walimu kuwa ilikuwa maandalizi ya Waheshimiwa kutukana na ikiwezekana wapigane humohumo Mjengoni tusiwone. Tv zingewazingiwa.
 
Kwaujumla sikutaka kuendelea kujadili hilo au kujibu tena.
Nilishikwa na mawazo makubwa hasa nikizingatia umuhimu wa Bunge kuwa ni Mhimili mmojawapo kati ya ile mitatu. Namaanisha jukumu lao kubwa hasa la kuisimamia Serikali, na kutunga sharia ambayo hutafsiriwa na Mhimili wa Mahakama.
 
Watu hawa tumewachagu, tumewapigia kura ili kutekeleza  jukumu letu la Kidemokrasia. Sina uhakika wamekumbwa na pepo gani. Kuna baadhi wanasema PEPO mkubwa ni Uchama Tawala na Uchama pinzani. Sina uhakika pepo hilo linanguvu gani humo mjengoni awamu hii. Kwani Uchama Tawala ni watanzania na wale wenye Pepo la Uchama Pinzani ni watanzania. Wanandoto nchi isitawalike. Ndoto hii ikitimia ni kwa faida ya nani?
Tuache ushabiki, kamchezo haka ka kuporomosha matusi kakiendelea, Waheshimiwa hawa watakuwa wametuangusha wananchi wao kwa kutuvunjia heshima ndani na nje ya nchi.
Katika midani za kimataifa tutafedheheka hasa tukipima uzito wa vile tunavyoheshimika.
 
Naamini kuna wabunge wengi wazuri, wenye uwezo na karama kibao. Yafaa wabunge hao wachukue hatua za kuwasaidia wachache wenye ujuzi wa kuleta vurugu awe Mwenye pepo la Utawala au Pepo la Upinzani kuacha kuutoboa mtumbwi wa Bunge la Tanzania kwa faida ya walipa Kodi wanaopinda migongo mashambani na maeneo mengine ya uzalishaji.
 
 Wakumbuke uchaguzi haupo mbali, wakumbuke kizazi hiki ndiyo kile baadhi yao wameshafeli shule za Sekondari za kata. Wanasota bila kusikia wabunge wao kujadili namna watakavyowaokoa. Wanahasira. hasira zao ni kwenye sanduku la KURA.
 


UJUMBE WA JUMAMOSI TOKA KWA DADA YASINTA WA MAISHA


KIJANA WA DADA YASINTA (KUSHOTO)  WALIPOTEMBELE OFISI YETU  RURAL PRESS, SONGEA ILIYOPO UWANJA WA SABASABA-MATARAWE SONGEA AKIWA NA WAZAZI WAKE (HAWAPO PICHANI) AMEKAA NAMI JUMA NYUMAYO. MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO NILIFURAHI SANA FAMILIA HIYO KUTUTEMBELEA OFISINI NA KUJIFUNZA TUFANYAYO.
Nimekuwa msomaji wa marakwa mara wa Blogu ya MAISHA ruhuwiko.blogspot.com, na VANGONI zote hizo za Dada yetu Mpendwa Yasinta Ngonyani anaeishi Sweden. Yasinta na familia yake tumewahi kuonana machokwamacho. Watoto wa siku hizi wanasema "live." Tulizungumza mengi. Kilichonifurahisha katika hayo mengi ni pamoja na ujumbe huu wa Jumamosi ya Leo, Siku moja tu kabla ya kuadhimisha siku yangu ya kuzaliwa hapo kesho Tarehe 21, Aprili.
Ninajivunia Dada Yasinta kwakuwa mmojawapo aliyejiunga na Blogu yangu ya "Jamii ya wana Ruvuma" www.http//ruvumapress.blogspot.com. mwanzoni na kuijumuisha katika Blogu anazozifuatilia. Asante saana Dada    

Ujumbe wa Jumamosi nimeuchukua Katika Blogu yake ya www.http//ruhuwiko.blogspot.com  na ukibonyeza tu hapo utakumbana na "kisima cha maarifa."  Utafaidi.

Namuomba radhi kwa kuchukua ujumbe wake huu, naamini ataikubali kwakuwa lengo lake tunufaike wote. Asante Dada Yasinta.

Ukiwa DUNIANI USIHUZUNIKE na usiwe MNYONGE hata kama una UMASKINI kiasi gani. Mungu yuko pamoja nawe na unatakiwa kuzingatia haya:-
1. Usijilaumu kwa lolote lililokutokea
2. Usihofu kuhusu hali uliyo nayo sasa.
3. Usijilinganishe na mtu yeyote duniani.
4.
5. kumbuka Mungu ndie mpangaji wa kila linalokutokea.
6. Usiwaze sana kuhusu kesho waza kuhusu leo.
7. Ukikosa ulichokikusudia yote ni mipango ya Mungu.
MUWE NA SIKU/JUMAMOSI  NJEMA

NGOMA YA MASHUJAA WA KINGONI (LIGIHU) V/S NGOMA ZA KUFOKAFOKA


AFISA  SEKRETARIETI YA MKOA RUVUMA,  BW HUMPHREY V.  PAYA (KUSHOTO) AKIWA NA BALTHAZAR NYAMUSYA, KAIMU MHIFADHI MKUU WA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI  ILIYOPO SONGEA, RUVUMA


WACHEZAJI WA NGOMA YA MASHUJAA WA KINGONI MAARUFU KAMA LIGIHU WAKITUMBUIZA SIKU YA MASHUJAA FEB. 26, 2013. WANAPENDEZA KWA MAVAZI NA KUCHEZA LAKINI HAKUNA  WATOTO WALA VIJANA WANAOJIFUNZE NGOMA HIYO MUHIMU KWA  MILA NA KABILA LA WANGONI NA MAKUMBUSHO HAYO KUSINI MWA TANZANIA.


KATIBU HAMASA VIJANA MKOA WA RUVUMA NA MSHEREHESHAJI WA SHUGHULI MBALIMBALI  BW. KIPANDE, AKIANGALIA MWENENDO WA SHEREHE ZA MASHUJAA MAPEMA MWAKA HUU, WALIOKAA CHINI WAMEJIFUNGA VILEMBA VYEKUNDU NA T-SHIRTS NYEUPE NI KIKUNDI CHA NGOMA YA BETA CHA LIZABONI MANISPAA YA SONGEA.


WAHESHIMIWA MADIWANI WA MANISPAA YA SONGEA, (TOKA KUSHOTO WALIOKAA) MHE. REHEMA MILINGA (VITI MAALUM  - CCM), MHE. GENFRIDA HAULE (VITI MAALUM-CCM), MHE. VICTOR NGONGI DIWANI KATA YA RUVUMA NA MHE. MAURUS LUNGU DIWANI WA KATA YA MLETELE. ALIYESIMAMA NI MWANDISHI WA HABARI GAZETI LA MAJIRA, MHAIKI ANDREW SIKU YA MAADHIMISHO KUMBUKIZI KUNYONGWA KWA MASHUJAA WA VITA VYA MAJIMAJI MAPEMA FEB, 26 2013.


VIJANA WA SONGEA HOUSE OF TALENTS WAKIFANYA VITU VYAO IKIWA NI PAMOJA NA KUMWAGA RADHI, WALITUZWA ZAIDI YA SHILINGI 70 ELFU PAPO HAPO AKIONGOZA MGENI RASMI WA MAADHIMISHO HAYO WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,  MHE. BALOZI HAMIS KAGASHEKI. KUNA UMUHIMU WA MAKUNDI KAMA HAYA YAKAJIFUNZA PIA NGOMA KAMA LIGIHU NA NYINGINE KIBAO BADALA YA KUFOKAFOKA TU. 
.

Friday, April 19, 2013

BARABARA ZITAPONA KWELI KWA MATUMIZI YA KUSAFIRISHA MAKAA YA MAWE? ANGALIA MALORI HAYO


MAGARI MAKUBWA YANAYOTUMIA BARABARA YA MAKAMBAKO - SONGEA - NGAKA KUSAFIRISHA MKAA  KAMA YANAVYOONEKANA LEO HAPO ENEO LA LIZABONI MANISPAA YA SONGEA HADI RUHUWIKO MANISPAA YA SONGEA.





 


PICHA  ZA MALORI YALIYOEGESHWA KANDO YA BARABARA, BAADHI YA WACHUNGUZI WA MAMBO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA  HAWANA UHAKIKA WA USALAMA WA BARABARA HIZO LICHA YA KUWA ZA KIWANGO CHA LAMI. MAKAA YA MAWE YANAYOENDELEA KUBEBWA KWA MALORI KWA KUTUMIA BARABARA YA MAKAMBAKO -SONGEA ILIYOZINDULIWA MWISHONI MWA MIAKA YA 1980 INA  UMRI MKUBWA KUHIMILI UZITO NA  HUENDA IKAHARIBIKA VIBAYA KATIKA KIPINDI HIKI CHA USAFIRISHAJI WA MAKAA HAYO.
IPO HAJA YA KUANZISHA RELI NA KIASI CHA MAKAA MENGINE KUZALISHA UMEME HUKOHUKO KIJIJI CHA NGAKA MBINGA.


CHADEMA KUHUSISHWA NA UGAIDI SOMA HAPA

 
Kwa siku kadhaa ndani ya vikao vya Bunge la Tanzania linaloendelea sasa, kumezuka malumbano kati ya vyama vya CCM (tawala) na  CHADEMA (upinzani)  wakati wa kujadili suala la ugaidi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba alikituhumu CHADEMA kuwa ndicho kinachopanga ugaidi wa ndani ya nchi.

Mbunge Tundu Lissu wa CHADEMA hakufurahishwa na matamshi hayo na akaamua kujibu kwa kusemakuwa Ikulu ya Rais ndiyo inayopanga ugaidi wa ndani ya nchi. 

Ili kujua zaidi kuhusu tuhuma hizo, mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya Radio Iran, Teheran bwana Salim Swaleh alizungumza na Tundu Lissu. Iliyopachikwa hapa ni  sehemu ya mazungumzo hayo.


Source: http://www.wavuti.com/

WASIWASI WA MAISHA BAADA YA MLIPUKOMASHINDANO YA MARATHON BOSTON MAREKANI


Nimeamshwa na simu kutoka Emergency Alert ya mji wa Cambridge, MA wakisema kuwa ni marufuku kutoka nje ya majumba yetu leo! Hakuna usafiri, wameomba sehemu za kazi zisifungue!

Wanasema kuwa hakuna kufungua mlango hata kama ni polisi, wanasema kuwa jamaa anataka kuua watu!

Jana usiku ilikuwa balaa hapa Cambridge! Cambridge ni nje ya Boston.  Kwanza kwenye saa tatu na nusu (9:30PM) tulisikia kuwa majambazi walivamia duka la  7-11 Central Square!

Kukaa kidogo tukasikia Polisi kapigwa risasi Chuo Kikuu cha MIT! Baada ya muda mfupi wakasema yule polisi kafa!

Kwenye saa tano tukasikia mtu kaibiwa gari yake aina ya Mercedes Benz, kwenye kituo cha mafuta!  Ni mwendo mfupi toka ninapokaa! Nikaanza kusikia milio ya gari ya polisi!

Kumbe polisi wa kila aina walikuwa wanawafukuza  karibu na Arsenal Mall. Milio ya risasi balaa, ambulance na magari ya polisi yalikuwa yanafukuzana, kwenye TV, tukaona kila mtu aliyefanana na Mspanish, Mwarabu kasimamishwa na kusachiwa!

Sikulala hadi saa nane na nusu! Nimeamshwa na simu ya Emergeny Alert!


Source: http://www.wavuti.com/

HONGERA INVIOLATHA KWA KUPATA MTOTO



MISS INVIOLATHA MBUYA, MTUMISHI WA WAKALA WA VIPIMO ( WMA) SONGEA-RUVUMA, AWALI ALIKUWA VALONGO INTERNET CAFE,  SONGEA AMEPATA MTOTO WA KIKE.
 PICHANI INVIOLATHA AKIWA AMEMSHIKA MTOTO WAKE  MBELE YA KANISA KUU LA PERAMIHO MKOANI RUVUMA HIVI KARIBUNI.

MTOTO  BERNADETHA (NYANGETA)  ALIYABATIZWA HIVI KARIBUNI HAPO PERAMIHO  ANAONEKANA KATIKA POZI TOFAUTI  KAMA ILIVYOHAPO CHINI.



MISS INVIOLATHA AKIWA KATIKA POZI BAADA YA KUJIFUNGUA NA KUTOKA NDANI NA MWANAE