Pages

Saturday, April 20, 2013

PEPO GANI KAINGIA MJENGONI?


JENGO LA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LILILOPO DODOMA.


Na Juma Nyumayo, Songea.
 
MJADALA Mkubwa umeibuka katika nchi ya Tanzania kuhusu kinachoendelea katika Bunge huko Dodoma.
Mjadala huu umechukua sura ya namna yake  kutokana na Matusi ya nguoni, kejeli, dharau na kile kinachotafsiriwa na watu wa makundi mbalimbali kuwa wabunge hao wameacha walichoendea Dodoma.
Hivi sasa, katika ngazi ya familia, mjadala huo umechukua sura ya watoto na wazazi wao au walezi kupeana majina kuwa wasifanye kama waheshimiwa wafanyavyo mjengoni.
 
Kwaujumla, Wabunge wamewaangusha wapiga kura wao. Namaanisha hata wabunge amabao hawajawahi kufunua midomo yao tangu waingie Mjengoni hapo, hawakwepi lawama hii.
Mwanafunzi mmoja aliniuliza nikiwa kama Mwandishi wa habari.
Mwanafunzi: Eti waheshimiwa wabunge walikuwa hawataki Bunge lioneshwe "live" ili watukane?
 
Mimi: Wewe umemsikia nani?
Mwanafunzi: Wanasema baadhi ya walimu kuwa ilikuwa maandalizi ya Waheshimiwa kutukana na ikiwezekana wapigane humohumo Mjengoni tusiwone. Tv zingewazingiwa.
 
Kwaujumla sikutaka kuendelea kujadili hilo au kujibu tena.
Nilishikwa na mawazo makubwa hasa nikizingatia umuhimu wa Bunge kuwa ni Mhimili mmojawapo kati ya ile mitatu. Namaanisha jukumu lao kubwa hasa la kuisimamia Serikali, na kutunga sharia ambayo hutafsiriwa na Mhimili wa Mahakama.
 
Watu hawa tumewachagu, tumewapigia kura ili kutekeleza  jukumu letu la Kidemokrasia. Sina uhakika wamekumbwa na pepo gani. Kuna baadhi wanasema PEPO mkubwa ni Uchama Tawala na Uchama pinzani. Sina uhakika pepo hilo linanguvu gani humo mjengoni awamu hii. Kwani Uchama Tawala ni watanzania na wale wenye Pepo la Uchama Pinzani ni watanzania. Wanandoto nchi isitawalike. Ndoto hii ikitimia ni kwa faida ya nani?
Tuache ushabiki, kamchezo haka ka kuporomosha matusi kakiendelea, Waheshimiwa hawa watakuwa wametuangusha wananchi wao kwa kutuvunjia heshima ndani na nje ya nchi.
Katika midani za kimataifa tutafedheheka hasa tukipima uzito wa vile tunavyoheshimika.
 
Naamini kuna wabunge wengi wazuri, wenye uwezo na karama kibao. Yafaa wabunge hao wachukue hatua za kuwasaidia wachache wenye ujuzi wa kuleta vurugu awe Mwenye pepo la Utawala au Pepo la Upinzani kuacha kuutoboa mtumbwi wa Bunge la Tanzania kwa faida ya walipa Kodi wanaopinda migongo mashambani na maeneo mengine ya uzalishaji.
 
 Wakumbuke uchaguzi haupo mbali, wakumbuke kizazi hiki ndiyo kile baadhi yao wameshafeli shule za Sekondari za kata. Wanasota bila kusikia wabunge wao kujadili namna watakavyowaokoa. Wanahasira. hasira zao ni kwenye sanduku la KURA.
 


No comments:

Post a Comment