Pages

Tuesday, April 30, 2013

GONGO YAMPELEKA KUZIMU MWALIMU MSTAAFU



Mtambo wa Pombe ya Moshi maarufu kama 'Gongo'


Na Steven Chindiye, Tunduru
MWALIMU mstaafu katika Kijiji cha Kidodoma Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma, Rajab Mohamed, Kalesi (65) amefariki dunia baada ya kunywa pombe haramu ya Moshi ambayo inafahamika kwa jina la Gongo.
Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mdogo wa marehemu Athuman Saidi, walisema kuwa kabla ya mkasa huo marehemu alionekana akinywa Pombe hizo kwa siku mbili mfululizo akiwa amefungiwa katika nyumba ya muuzaji wa pombe hiyo Hamdi Swalehe huku akiwa anatamba kuwa ana fedha nyingi alizokuwa ametoka kulipwa kama mafao ya kustaafu kazi hiyo.
Walisema kufuatia taarifa hiyo ya kupokea fedha hizo zinazo daiwa kuwa zilikuwa ni zaidi ya Shilingi Milioni 48 mstaafu huyo alionekana kutembea na wapambe muda wote huku wakienda kujipatia kinywaji hicho kwa wingi na kumsababishia dhahama hiyo ya kupatwa na umaiti.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Diwani wa viti maalumu wa Tarafa ya Nampungu Rehema Nyoni na Mtendaji wa Kijiji hicho Mbuyu Ally Mbuyu walisema kuwa baada ya wapambe hao kuona hali ya tajiri yao imebadilika walitimua mbio na kumtelekeza katika nyumba ya muuza pombe hiyo hadi umauti ukamkuta akiwa peke yake.


Walisema akiwa katika hali yha kutapatapa Mke wa muuza pombe hiyo alijitahidi kuokoa maisha yake kwa kumpatia huduma ya kwanza kwa kumpepea, kummwagia maji ya baridi na baadae akamnywesha uji lakini hali ilizidi kuwa tete na alipo kata roho mumewe Hasani Swalehe alitimua mbio na kumwacha marehemu akiwa juani.


Akizungumzia tukio hilo Mganga aliye ufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Kalesi Dkt, George Chiwangu alisema kuwa chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na unywaji wa pombe nyingi.


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kufuatia hali hiyo wanamshikilia mke wa muuza pombe huyo ambaye hakumtaja jina lake kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment