Pages

Tuesday, October 11, 2011

Vibaka wanaoiba viporo vya wali wapungua



Hakika Songea ina mambo! leo nimetembelea maeneo ya Matarawe hapa Songea Mjini, na kuambulia hadithi hii hapa chini! Hongera zake RPC Kamuhanda Pichani










Eti wakazi wa eneo hilo wanashangilia kupungua kwa vibaka ambao Usiku huingia majumba ya watu na kula vipolo vya wali. wakazi wa eneo hilo wanasema wanashukuru sana falsafa ya ulinzi shirikishi au kwa jina maarufu Polisi Jamii chini ya Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda kuwa sasa vibaka hao wamepungua.

Mkazi mmoja kaniambia pia eti Yeboyebo yaani Pikipiki zinazosafirisha abiria zimesaidia kutoa ajira na kuwafanya vijana wengi kuacha wizi wa viporo vya wali au ugali majumbani mwa watu katika Mitaa ya Bombambili, Mjimwema, Mfaranyaki, lizaboni na ile ya katikati Mjini hapa kama Mfaranyaki na Misufini bila Kusahau majengo.





1 comment:

  1. Aise! kaazi kwelikweli kuyiwa ugali na wali kabisa sasa hii ni kali.

    ReplyDelete