Pages

Thursday, September 22, 2011

CHADEMA YAKACHA KUMSIMAMISHA MGOMBEA UMEYA!

Chama cha Upinzani kilichochukua Kata tano Muhimu kati ya 21 katika Manispaa ya Songea,CHADEMA kimekacha kumsimamisha Mgombea katika Uchaguzi wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Siku ya Ijumaa Septemba 23, mwaka huu kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mstahiki Meya Ali said Manya aliyefariki na Kuzikwa nyumbani kwake Lizaboni mjini hapa. Mheshimiwa Manya alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea baada ya Ushindi katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 na kuchaguliwa kuwa Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Lizaboni.
Chama cha Mapinduzi CCM ndiyo pekee kimemteua Mheshimiwa Charles muhagama Diwani wa Kata ya Matogoro kugombea Nafasi hiyo muhimu. Hivi sasa Manispaa ya Songea ipo chini ya Naibu Meya Mariam Dizumba mheshimiwa Diwani Viti maalum. Juu pichani wanaonekana Mheshimiwa Charles Muhagama (kushoto) akiteta jambo nje ya Ukumbi wa Songea Club na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Songea Mheshimiwa Ali Said Manya na Marehemu Adam Ngongi maarufu Mzee Yapenda ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya SOUWASA. Ilikuwa Julai 20, 2010 wakati wa kusaini Mkataba mkubwa wa kuendeleza Programu ya maji.

No comments:

Post a Comment