Bw Kindamba Namlia (Pichani) Mtangazaji anayechipukia na kupendwa sana na wasikilizaji wa Jogoo FM- Songea Radio inayopasua mawimbi hadi Msumbiji. hata hivyo Kindamba naandika haya hapa chini kama wito kwako:
MIMI Kindamba naomba ushirikiano na wasikilizaji na wadau wa JOGOO FM- SONGEA Radio changa inayoleta changamoto za kimaendeleo ya Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni mkoani Ruvuma na mikoa ya jirani kama Mbeya, Njombe, Morogoro, Iringa na Katavi pia kule Rukwa bila kusahau Msumbiji.
utangazaji unachangamoto nyingi. naishukuru Blog ya Jamii ya wanaRuvuma kwa kazi nzuri.
Maneno hayo ni ya Kindamba alipofika Ofisini kwangu leo. nami nampa shavu kwa kibarua alichokianza hapa Songea.
(Juma NYumayo)
Pages
▼
Friday, February 18, 2011
CHADEMA WALIPOTEMBELEA RUVUMA PRESS KUJENGA UHUSIANO
VIONGOZI wa CHADEMA wilaya ya Songea na MKOA wa RUVUMA wakiwa mbele ya Ofisi za RUVUMA PRESS CLUB wa kwanza na wa pili kushoto ni waandishi wa habari na watatu ni Diwani wa Majengo kupitia Chadema Mhe. Iddi Abdalah. Hawa wanajua wanachokifanya hasa baada ya kushinda kata 5 manispaa ya Songea na Kupata mgao wa Madiwani viti maalum wawili hao waliochuchumaa toka kulia Mhe Rhoda Komba na wa katikati anayeitwa Grace.
Mnara utakaozinduliwa waliponyongwa Mashujaa wa Majimaji
Nikiwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi, Picha hiyo unayoiona tayari sasa kimekuwa kitu halisi. MNARA uliojengwa na VETA-Songea nyuma ya Ukumbi wa Songea Club pale waliponyongwa mababu zetu kupinga kutawaliwa na Wajerumani. Pamependeza kwelikweli. Mnara umebeba kinjenje, chibonga (Rungu) Mgoha (Mkuki) Chikopa (Ngao) na Juu kabisa Mwenge ishara ya nuru yenye matumaini. Nitakuletea unavyoonekana kama nilivyoupiga picha jioni leo.
Da siku nyingi sikuwepo hewani!
Hapa Juma Nyumayo Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club akimwelekeza jambo Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Bw Michael Kamuhanda katika viwanja vya makumbusho ya taifa ya Majimaji Mjini Songea ambapo juma hili wageni kadhaa wenye hadhi tofauti watahudhuria maadhimisho ya Tamasha la kitaifa la Utalii wa Kiutamaduni katika mji wa Kishujaa na Kihistoria wa Songea. Tamasha hilo linakwenda sambamba na Kumbukizi za kunyongwa viongozi wa kingoni miaka zaidi ya 1oo iliyopita.