Pages

Friday, February 18, 2011

Mnara utakaozinduliwa waliponyongwa Mashujaa wa Majimaji

Nikiwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi, Picha hiyo unayoiona tayari sasa kimekuwa kitu halisi. MNARA uliojengwa na VETA-Songea nyuma ya Ukumbi wa Songea Club pale waliponyongwa mababu zetu kupinga kutawaliwa na Wajerumani. Pamependeza kwelikweli. Mnara umebeba kinjenje, chibonga (Rungu) Mgoha (Mkuki) Chikopa (Ngao) na Juu kabisa Mwenge ishara ya nuru yenye matumaini. Nitakuletea unavyoonekana kama nilivyoupiga picha jioni leo.

1 comment:

  1. mwenga nihekili kweli unikumbusi kunyumba kicnjenje, chibonga,mgoha na chikopa:-) Tupo pamoja!!

    ReplyDelete