Pages

Wednesday, February 3, 2016

Narudi tena katika Blogu,

Ama kweli, teknolojia  imekuwa kwa kasi kubwa.
Facebook, tweeter, na whatsApp viliniondoa kwa muda mtefu hapa.
hata hivyo nimeamua kurudi tena na kuendelea kupashana habari kama hobby.
Awali ya yote habari za mwaka mpya 2016. Kwa watanzania tunamshukuru mungu, maana serikali ya awamu ya tano ya Rais,  Dkt. John Pombea Magufuli, inaendelea kwa kasi kutumbua kila aina ya majipu, hata kama ni jipu chungu litatumbuliwa tu maana falsafa hapa ni ile ya HAPA KAZI TU! Elimu bure watoto wengi wameandikishwa madarasa ya awali na la kwanza. Sekondari ndiyo usiseme , Kumbe kweli umasikini na michango lukuki ya kuchangia elimu ilikuwa si kero tu bali kikwazo cha kusomesha watoto kwa wazazi na walezi waliowengi. Asante Dkt. Magufuli.
Mpaka siku nyingine tupo pamoja.