Pages

Thursday, December 26, 2013

Mwanahabari Mkongwe Adam Mzuza Nindi afunguka


Mwanahabari Mkongwe, Mwakilishi wa Radio Free Africa na Star TV Mkoani Ruvuma, Bwana Adam Mzuza Nindi,  Amefunguka na tathimini ya kazi katika Blogu 
Haya hapa chini ndiyo Maneno  yake na picha hapo juu alipost katika Blogu yake ya : www. songeahabari.blogspot.com
  
Uchunguzi wa Habari za kuwa wafaa wananchi ni mhimu sana ,Hebu Tuone sasa tuna Maliza Mwaka yepi mazuri yaliyo fanywa na Wandishi wa Habari na Yepi mabovu yaliyo fanywa na Waandishi wa Habari. Tujitathini wenyewe tusipige katumba kuonyesha vidole kwa wenzetu Pale tulipo kosea tuji sahihishe na Pale tulipo fanya vizuri tuboreshe zaidi Bado siku chache za kumaliza Mwaka lakini lazima Waandishi Tujipange Hapo ni Mwandishi Mwandamizi Juma Nyumayo (aliyesimama) akiwa na Mkongwe wa Habari Adam Mzuza Nindi wakitathiminji mwaka 2013

Wednesday, December 18, 2013

LAKE OIL LTD KUFUNGUA MAUZO YA MAFUTA SONGEA

Mtumishi wa lake Oil Ltd, Bw. Moses Clemency, akiwa mbele ya moja ya Pampu mpya za mafuta katika Kituo hicho kilichopo eneo la Manzese, Manispaa ya Songea.

KAMPUNI ya mafuta Lake Oil Ltd ya Dar es Salaam, imefungua Kituo cha mafuta Manispaa ya Songea.

Kituo hicho kilichopo Mkabala na Ofisi za Zimamoto na kuangaliana na Soko la Wakulima Manzese mjini hapa, kimebadili Sura ya eneo hilo kutokana na Ukarabati na kujenga paa kubwa katika Pampu mpya za mafuta aina ya Diesel, Petroli na ya taa.

Kwa Mujibu wa Meneja wa Kituo hicho, Bw. Daud Mmasa Sevuri, alisema kuwa huenda Alhamisi wiki hii wakaanza kuuza mafuta kwa bei nafuu wakilinganisha na vituo vingine mjini hapa.
"Alhamisi wiki hii tunatarajia kuanza kuuza mafuta hapa songea," alisema.

Ujio wa Kampuni ya Lake Oil Mkoani hapa, utaongeza ushindani wa Biashara ya mafuta ya mitambo na Gas kwa matumizi mbalimbali na kusaidia kusukuma maendeleo ya sekta ya kilimo, madini, usafiri na utoaji huduma.

Mkoa wa Ruvuma haujaunganishwa na Umeme Grid ya taifa hivyo kuufanya kutegemea zaidi mafuta.
Kilio kikubwa cha wakazi wa mkoa huu kitabaki kupata wakala wa kuuza mafuta ya ndege.
Angelipatikana wakala huyo Uwanja wa ndege ulioko eneo la Ruhuwiko manispaa ya Songea, wenye ubora wa kutua ndege mbalimbali isipokuwa Boeng,  ungeweza kutumika ipasavyo kwa abiria na kupunguza gharama ya nauli wanayolipa sasa kwa kutumia ndege ndogo.

Tuesday, December 17, 2013

WABUNGE 160 WA CCM WALIA NA MAWAZIRI MIZIGO

Ukumbi wa Bunge, Dodoma
                                  DODOMA/DAR ES SALAAM.                                                                                                                                                                                                                                                                    WABUNGE 160 wa CCM wamejiorodhesha kuomba kuitishwa kwa kikao cha Kamati ya Wabunge hao kwa lengo la kuwajadili mawaziri wanaotajwa kuwa mizigo.

Pia wabunge hao wanataka Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahaman Kinana naye awepo kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Hussein Mussa Mzee, alimwambia mwandishi wetu kuwa wamepokea barua iliyoambatana na orodha ya majina ya wabunge zaidi ya 160 waliotia saini kutaka kuitishwa kwa kikao hicho.
“Hata kama wangesaini wabunge 10 tu tungeitisha kikao. Bahati nzuri walisaini zaidi ya 160, kwa hiyo kikao kitaitishwa kwa kuwa ni haki yao kikanuni kutaka kukutana,” alisema.
Alipoulizwa kwa nini kikao hicho hakikuitishwa ndani ya wiki moja ambao ndiyo muda wabunge hao walioutaka kabla ya Kamati Kuu ya CCM kukutana wikiendi iliyopita, Mzee alisema hiyo lilitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kutokuwapo bungeni.
Mzee alisema pia kikao hicho kilishindwa kufanyika mara ya kwanza kutokana na Kinana kuwa safarini Afrika Kusini ambako alihudhuria mazishi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Hata hivyo, alisema hawezi kujua ni lini kikao hicho kitafanyika lakini aliahidi kuwa itakuwa mara baada ya Kinana kurejea nchini.
Wiki iliyopita, gazeti hili liliandika kuhusu wabunge wa CCM kujiorodhesha ili kushinikiza kufanyika kwa kikao hicho.
Chanzo kimoja cha kuaminika kilisema kuwa fomu hiyo iliwasilishwa katika Ofisi ya Katibu wa Wabunge wa CCM ikiambatana na barua inayotaka kuitishwa kwa kikao kitakachowakutanisha.
“Tuliwaomba waitishe kikao cha wabunge wa CCM ili mawaziri ambao tunawaona hawatimizi majukumu yao kikamilifu waweze kuhojiwa lakini wakawa wanasuasua,” kilisema chanzo hicho.
Kikao hicho kilitakiwa kufanyika Alhamisi iliyopita ili kuwahoji mawaziri hao kabla ya kikao cha Kamati Kuu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikaririwa wikiendi hii akieleza kuwa mawaziri saba walihojiwa katika kikao cha Kamati Kuu na kumuachia Rais Jakaya Kikwete jukumu la kuamua kuwafukuza kazi, kuwahamisha au kuwataka kutekeleza majukumu yao kikamilifu. MWANANCHI

Monday, December 16, 2013

Simulizi ya Mandela

Toka kulia: Rais wa sasa Afrika kusini, Jacob Zuma , Rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini,  Mzee Nelson Mandela (enzi ya uhai wake) na Rais wa pili wa Afrika Kusini,  Thabo Mbeki

Ndugu Zangu. 
Nahitimisha simulizi za Mzee Wetu Madiba. Najisikia nimechukua jukumu langu la kugawana nanyi kile kidogo nilichoweza kukusanya kumhusu Mzee wetu Madiba.


Natumaini nitapata muda siku zijazo, nisimulie zaidi juu ya yale yenye kufanya maisha ya Madiba kuwa simulizi endelevu kwetu Waafrrika na watu wa dunia. 


Lakini, ukweli unabaki, kuwa leo dunia imemzika Mzee Madiba kijijini kwao Qunu. Yaliyobaki nyuma yake ni yale mema aliyoishi akayahubiri. Nasi tunapaswa kujifunza kutoka hayo.
Yumkini Mungu amechagua kupumzisha Mandela wakati muafaka. Maana, ni katika kipindi ambacho, Afrika Kusini inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwakani.



Chama kikuu cha ANC kinakabaliwa na changamoto za ndani ya chama na kwenye jamii. Kinapaswa sasa kijiandae kufanya mabadiliko makubwa yatakayorudisha imani ya wapiga kura wake wengi. Wapiga kura ambao wameanza kukata tamaa. Hawana furaha ya maisha yao. Wamekata tamaa ya kuona kuwa kesho yao yaweza kuwa bora zaidi.



ANC kihistoria imekuwa ikitegemea sana Jumuiya yake ya Vijana na Shirikisho la Wafanyakazi ( Cosatu) Jumuiya zote hizo zinaonekana kugawanyika. Kuna wanaoipa mgongo ANC. 


Na Mandela anausia; 
" The leader must keep the forces together, but you can't do that unless you allow dissent. People should be able to criticise the leader without fear of favour. Only in that case are you likely to keep your colleagues together"- Nelson Mandela. It is when Mandela gave a piece of advice to newly elected Party Leader, Thabo Mbeki at the ANC Congress in Mafikeng, 1997. 



Kwamba kiongozi unapaswa kuyaunganisha makundi, lakini, huwezi kufanya hivyo kama huruhusu sauti kinzani. Sauti za wenye kukupinga. Watu wawe huru kumshutumu kiongozi bila ya woga. Ni kwa namna hiyo tu kiongozi unaweza kuyaunganisha makundi. Mandela aliyasema hayo kule kwenye Mkutano Mkuu wa ANC uliompitisha Thabo Mbeki kuwa Rais wa ANC, ni mwaka 1997. 

Naye Askofu Desmond Tutu alipata kusema; 
"Kuna tofauti ya kimsingi kati ya kuwa huru na kuwa katika hali ya kukandamizwa. Kuwa huru ni pamoja na kupata huduma za msingi za kijamii, kuwa na ajira, maji ya bomba, umeme, makazi bora na huduma za msingi za afya. Kuna maana gani basi ya kuwa huru wakati ubora wa maisha ya watu haujaimarishwa? Kama sivyo, hata kura nazo hazina maana yoyote!" (Desmond Tutu- William Gumede; Thabo Mbeki And The Battle For The Soul Of The ANC, Uk. 67). 

Nkosi Sikelel i Afrika


Kwa hisani ya Juma Mtanda

WAPINGA MAENDELEO YA ELIMU MBINGA KUKIONA


Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Senyi Ngaga akitoa msisitizo wake mbele ya Wadau wa elimu wa wilaya hiyo(Hawapo pichani) katika ukumbi wa Umati uliopo mjini hapa, juu ya Katibu wa CWT wilaya humo kuwa ni kikwazo cha maendeleo ya elimu. 


Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

MKUU wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Senyi Ngaga amemshukia Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) tawi la Mbinga Samwel Mhaiki, akidai kwamba ni kikwazo cha maendeleo ya elimu wilayani humo, kutokana na katibu huyo kupenda kuendesha migogoro na kuchonganisha walimu mashuleni.

Ngaga alisema hayo alipokuwa akizungumza na Wadau wa elimu, Kata ya Mbinga mjini juu ya kukuza maendeleo ya sekta ya elimu wilayani humo, katika hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa Umati uliopo mjini hapa.

Alisema kuwa katibu huyo amekuwa kinara namba moja wa kupita mashuleni na kushinikiza walimu waache kufundisha (Wagome) hadi watakapolipwa madai yao, jambo ambalo alilieleza kuwa limekuwa likileta mgogoro usio na tija katika jamii.

Alieleza kwamba licha ya Mhaiki kuitwa mara nyingi ofisini kwake na kumtaka aache kuendeleza migogoro hiyo, anashangaa kumuona bado akiifanya.


“Tumemuonya mara nyingi huyo Mhaiki, lakini amekuwa bado akitusumbua kwa kuandika mabarua na kusambaza mashuleni akishinikiza walimu wagome waache kufundisha….tulimwambia serikali inashughulikia madai ya hawa walimu na watalipwa malumbano haya anayoyaendeleza sasa ningelikuwa na uwezo mimi kama Mkuu wa wilaya hii ningemhamisha, kwa sababu ni kikwazo kwa maendeleo ya elimu hapa wilayani, leo walimu wakigoma watoto wetu watafundishwa na nani”, alisema Ngaga.

Mkuu huyo wa wilaya awali alisema wilaya hiyo hivi sasa imejipanga katika kukuza kiwango cha elimu kwa shule za msingi na sekondari, ambapo kwa kushirikiana na ofisa elimu wa wilaya hiyo Mathias Mkali wamekuwa wakiendelea na mfumo wa watoto kujisomea wakati wa likizo (Makambi) kwa kila kata wilayani humo, hususani kwa watoto wa darasa la sita ambao wanaingia darasa la saba mwakani.

Alisema wazazi wameitikia wito kwa kiasi kikubwa juu ya suala hilo na kukubaliana kutoa michango ya chakula, katika vituo hivyo ambavyo watoto wao wanasoma wakati huu wa likizo.

Alisisitiza kuwa mtu yeyote atakayeonekana anakwamisha mikakati waliyojiwekea ya kukuza kiwango cha elimu wilayani Mbinga, yupo tayari kumwajibisha ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo