Pages

Wednesday, July 10, 2013

SHULE YA SEKONDARI LONDON NA MAFANIKIO YAKE


 Mwanafunzi wa Kidato cha III 2013, Japhua Nyumayo, akiwa na Mzazi wake Hindu Said, wakisubiri kumuona Mkuu wa Shule  katika Ofisi Kuu ya Shule ya Sekondari ya Londoni iliyopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma leo.


Mbele ya Jengo la Utawala, Maua yamepandwa kwa mpangilio na kumwagiliwa vyema licha ya msimu huu wa kiangazi  kuwa na jua kali, maua hayo yanaendelea kupendeza na kuifanya shule kuwa ya kijani. Licha ya majengo ya Utawala, Madarasa, Vyoo na Mabweni kutunzwa vema bado ni somo tosha kwa wanajumuia wa shule hiyo na wanaowazunguka kujifunza utunzaji wa usafi na mazingira.


Alama ya Taifa, Bendera ikipepea katika Viwanja vya Shule hiyo ya Kidato cha I-VI ambayo inaendelea kujizolea sifa kitaaluma na nidhamu mkoani Ruvuma na kuwasukuma wazazi na walezi wengi kutaka vijana wao wahamie katika shule hiyo.
Shule hiyo hivi sasa ina Bweni kwaajili ya kulala wasichana. 


Mkuu wa Shule, Mwl. Christopher Mwageni, akiwa Ofisini kwake ambamo huendesha shughuli za utawala na uongozi.  Utawala wake uliojengeka imara kwa ushirikianao wa walimu, wanafunzi na watumishi wengine wa shule kwa msaada wa miongozo ya Bodoi ya Shule, umenyanyua jina la Shule ya Sekondari London  na kuiweka miongoni mwa Shule za  Sekondari za wananchi  bora zinazoiletea sifa serikali mkoani Ruvuma.


Mwalimu wa Shule ya Sekondari London,  Rashid Othman (Kushoto) akizungumza na mzazi wa Mwanafunzi wa shule hiyo .



Wanafunzi wavulana wa Kidato cha IV 2013 wakipata chai wakati wa mapumziko ya saa 4 leo, Jengo linalooonekana pale mbele ni jiko lao. Utaratibu huu wa Chakula shuleni unawawezesha vijana wengi kubaki muda wote shuleni na kuzingatia masomo yao.


No comments:

Post a Comment