Pages

Saturday, June 29, 2013

RAIS OBAMA AMZUNGUMZIA MZEE MANDELA


Rais Barak Obama amesema Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Mzee Nelson Mandela ameonyesha Uvumilivu na ujasiri na kwamba ni mtu wa kuigwa duniani.

Rais wa Marekani Barack Obama, amesema uvumilivu na ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na upendo wa dhati wa rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni kwa namna gani alivyo na utu wa kibinadamu.

Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha ukweli na ukakamavu ambao una maana kubwa katika utu wa kibinadamu ambao uliondoa tabaka la ubaguzi, udini na utaifa.

Rais huyo wa Marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria baada ya mazungumzo na rais wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
 
via/jumamtandablog

No comments:

Post a Comment