Pages

Thursday, June 13, 2013

POLISI ALIYEPIGA PICHA ZA UTUPU

NI kweli jamii yetu imekumbwa na ugonjwa wa kuporomoka maadili.
Hakika hukumu aliyoipata Polisi Amisa ya kufukuzwa kazi ni kali sana, ni fundisho sio kwake ni kwa wale waliopo Kazini
Yeye hayupo tena katika kazi hiyo, hivyo fundisho ni kwa waliopo kazini.

Hapa nakuja na hoja ya Picha zake kuanikwa hadharani baada tu ya kufukuzwa kazi katika Mitandao na baadhi ya Magazeti. Tishio.
Ndugu Mwanahabari, Msomaji tuangalie maswali haya:

Hebu vaa viatu vya Afande Amisa utajisikiaje?
uwe dada yake, kaka yake, mama yake, jirani, rafiki, Mtoto na mtu wa karibu wa afande huyo. Utajisikiaje katiak kusambaa kwa picha hizi baada ya tukio la kufukuzwa kazi.

Hebu tuwasikilize Askari wenzake, askari wanawake wanajisikiaje. Jibu la hili ni dhahiri kwa wanasaikolojia kuwa wameumizwa sana. Mimi kama Bloger picha zilitakiwa walao zingelizibwa usoni kupunguza madhara ya kibinadamu kwa hao niliowataja hapo juu. JADILI. 

Je kuna umuhimu wa kuendelea kuumiza waliomzunguka Afande amisa kwa kusambaza picha zake kama lengo ni kutibu mwenendo wa kimaadili?

No comments:

Post a Comment