Pages

Wednesday, June 5, 2013

PICHA ZAIDI ZA KUAGA MWILI WA MANGWEA DAR KUELEKEA MORO


Mwili wa marehemu Mangwair tayari kwa safari  ambapo umesafirishwa leo kuelekea Morogoro ambako maziko yake yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 06.06.2013 na msafara huu umehusisha watu mbalimbali wakiwemo wanakamati ya mazishi.
Kiongozi wa kamati ya maziko ya Marehemu Ngwair, Adam Juma, akitoa shukurani kwa watu mbalimbali walioshiriki kwa namna mbalimbali tangu mwili wa marehemu Mangwair ulipokuwa Afrika Kusini hadi kuuaga  leo mchana katika viwanja vya Leaders Club.
 
Hali ilivyokuwa baada ya zoezi la kuuaga mwili wa Mangwair kukamilika na safari  kuelekea Morogoro ikiwa inakaribia kuanza.

Watu hawaamini kilichotokea na wengine walitokwa na machozi hali iliyosababisha vilio kutawala.
Mwili wa Marehemu Mangair ukiangwa leo katika viwanja vya Leaders Club
Taratibu zikifanyika kuuweka vizuri mwili wa marehemu Mangwair
 
Sehemu ya umati uliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Mangwair katika viwanja vya Leaders Club leo mchana wakifuatilia kwa majonzi makubwa kinachoendelea

No comments:

Post a Comment