Pages

Tuesday, June 4, 2013

OMBENI FASTA MKOPO ELIMU YA JUU, MWISHO JUNI 30, 2013

 

Link kwa ajili ya kutuma maombi ya mkopo wa HESLB online ni: http://olas.heslb.go.tz


Mkurugenzi wa Mawasiliamo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu,  Cosmas Mwaisobwa amewataka waombaji wakamilishe ujazaji wa fomu hizo kabla ya Juni 30, 2013 ili kutoa nafasi kwa Bodi hiyo kuchambua maombi na kupanga madaraja.

Kuhusu wanaoendelea na masomo, Mwaisobwa alisema tayari waombaji 62,758 wamekamilisha taratibu za maombi ya mikopo na kujaza fomu stahiki tangu utaratibu huo ulipozinduliwa rasmi Mei Mosi mwaka huu.

“Hadi sasa mchakato kwa waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na wanafunzi wanaoendelea na masomo unaendelea vizuri ambapo wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa nia ya mtaandao,” amesema.

Katika mwaka wa masomo wa 2012/13, Bodi hiyo iliwapatia mikopo jumla ya waombaji 94,703, ambao wako katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu hapa nchini.

Idadi ya watakaopewa mkopo mwaka wa fedha 2013/14 haijajulikana hadi hapo bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itakapopitishiwa Bungeni.


Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment