Pages

Friday, June 7, 2013

MSIWAACHIE WATOTO KWENDA KWENYE KUMBI ZA STAREHE WAKATI HUU WA LIKIZO

WAZAZI na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi wameshauriwa kuwa karibu na watotowao ambao leo wamefunga shule kwa mapunziko muhula wa kwanza 2013.

"Wanafunzi hawa wanatakiwa wawe karibu na wazazi au walezi wao katika kipindi hiki cha likizo ya muhula wa kwanza," wadau wameuambia mtandao huu.

Wamesema kwa nyakati tofauti mjini hapa kuwa, watoto hao wakiachwa bila maelekezo sahihi watatumia muda huo kufanya mambo ambayo si sahihi. Aidha kwa wale wenye kumbi za video na kumiliki  kumbi za disco wasiwaruhusu watoto hao kuingia.

Naye  mwalimu wa siku nyingi  Mkoani Ruvuma, Nathan Mtega ameshauri watoto hao wapumzike na wasipelekwe kwenye mafunzo maarufu kama Tuition kwani watawachosha akili.

"hizi tuition wakati mwingine huwaletea mkanganyiko wanafunzi kwakuwa walimu wa tuition baadhi yao hawafuati mtaala na badala yake ni kukaririsha maswali na majibu tu," alisema Mwl. Mtega.

Alisema ni wakati muafaka kwa wazazi na walezi kuwatuma na kuwafundisha kazi ndogondogo  vijana hao kwa muda huu wa mapumziko.
Shule za msingi zimefungwa kuanzia leo Juni  7, hadi Julai 8, 2013.


No comments:

Post a Comment