Pages

Wednesday, June 19, 2013

KAHABA ATEMBEZEWA BAKORA DAR

Dar si mchezo, makahaba  waogope misikiti na makanisa. Angalia hasira za waumini.

  
Richard Bukos na Issa Mnally
 
KHAAA! Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ iliyo chini ya Global Publishes, ipo mzigoni na hivi karibuni imenasa tukio la aina yake ambapo mke wa mtu amechezea kichapo ‘hevi’ akidaiwa kufanya ukahaba jirani na msikiti, Risasi
Mchanganyiko lina kisa kamili.
 
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu majira ya usiku jirani na msikiti huo uliopo nyuma ya Corner Bar, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke huyo na wenzake walikamatwa na baadhi ya vijana waumini wa Kiislamu waliokerwa na kitendo cha wao kutoa huduma haramu ya ngono maeneo hayo.

WENZAKE WATOKA NDUKI
Baada ya wenzake kufanikiwa kutoka nduki mithili ya mwanariadha Usai Bolt wa Jamaika, mwanamke huyo alishuhudiwa akila bakora kisha akapelekwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama, Dar akaunganishwa na wengine waliokamatwa usiku huo.
 
Ilielezwa kuwa wanawake hao wamekuwa wakiuza miili kwa wanaume karibu na msikiti huo na pembezoni mwa baa hiyo.
 
Ilisemekana kuwa kumekuwa na kawaida ya wanawake hao kusimama maeneo ya nyumba hiyo ya ibada na kufanya biashara hiyo huku wakichafua mazingira kwa kutupa ovyo kondomu na kujisaidia maeneo hayo. 

NGUO YA NDANI YAMVUKA
Wakati mwanamke huyo akicharazwa bakora, nguo ya ndani ilimvuka huku akipiga kelele kuwa hatarudia kufanya hivyo na kama akirudia basi akatwe kichwa.

NI KERO
Kutokana na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti huo, waliamua  kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo hicho cha polisi.
 
“Tumeamua kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa, wanakojoa na kutupa kondomu  hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
 
Mmoja wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia mapaparazi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.

KUNA KISA NA MKASA
Alisema kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose kuhudhuria swala siku hiyo.

BOFYA HAPA KUSIKIA MAHOJIANO
Gazeti hili liliambatana na vijana hao hadi polisi ambapo lilipata nafasi ya kuzungumza na mwanamke huyo.
 
Risasi Mchanganyiko: Mama kwani wewe unaitwa nani na kwa nini unajiuza eneo lile ?.
 
Mwanamke: Naitwa Zulfa, unajua maisha ni magumu hata ninyi mnajua. Ni kweli mimi ni mke wa mtu lakini mume wangu hana kazi hivyo kuliko kulaza watoto njaa naogopa watakufa.
 
Risasi Mchanganyiko: Mume na watoto umewaacha wapi?
Zulfa: Mume naye anabangaiza mtaani, watoto wangu wawili nimewaacha nyumbani Manzese wamelala.
 
Risasi Mchanganyiko: Kwa nini usitafute njia nyingine ya kutafuta kipato kuliko kujiuza kwa sababu unahatarisha maisha na haya magonjwa ya siku hizi ?.
 
Zulfa: (kwa ukali), acheni maswali yenu kama mna hela nipeni nitaacha.

AINGIZWA LOKAPU
Hata hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.

NI SIKIO LA KUFA
Habari zilizolifikia gazeti ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.

DAR INATISHA
Biashara haramu ya ngono imekuwa kwa kasi ya ajabu jijini Dar na utafiti wa mwaka juzi ulionesha kuwa kulikuwa na wanawake wanaojiuza zaidi 7,500 lakini kwa sasa ni maradufu, chanzo kikielezwa ni ukosefu wa ajira.
NA GLOBAL PUBLISHER

No comments:

Post a Comment