Pages

Monday, June 3, 2013

ARDHI PLAN LTD YACHONGA BARABARA ENEO LA MRADI WA VIWANJA 18,000 MSHANGANO, MANISPAA YA SONGEA


Mhe. Diwani wa Kata ya Mshangano ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya Kata hiyo, Faustine Muhagama,  akimuonyesha Mwandishi maendeleo ya Uchongaji wa barabara za mitaa eneo la Mtaa wa namanyigu Kata ya Mshangano ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Upimaji wa Viwanja 18,000 uliofanywa na Kampuni binafsi ya Ardhi Plan Ltd toka Dar es Salaam. Mpango huo umebadili sura kabisa ya eneo hilo na kuwawezesha wananchi kumiliki na kujenga viwanja katika maeneo rasmishwa bila kupoteza mali zao na haki zao.
 
 

Mhe. Diwani Kata ya Mshangano, Faustine Muhagama (katikati) akionyesha mawe (Beacons) yakiwa karibu na Ofisi za Mtaa wa Namanyigu ambayo yatapandwa kwenye Mradi wa viwanja 18,000 Kata ya Mshangano inayohusisha mitaa mitatu ya Namanyigu, Mshanagano na Mitendewawa. Wengine ni Maofisa wa Kampuni Binafsi ya Upimaji Ardhi ya Ardhi Plan Ltd toka Dar es Salaam,  jana. 
 

Wataalamu wa wa Kampuni ya Ardhi Plan ltd, (toka kulia) Mpimaji (Surveyor) Emmanuel Mcharo na Fransis wakimuonyesha Mhe. Diwani wa Kata ya Mshangano, Faustin Muhagama, namba toka jiwe mojawapo kati ya mawe yatakayopandwa kwenye (Beacons)  mradi huo wa viwanja 18,000. Bw. Mcharo amesema kiasi cha mawe 30,000 yatapandwa katika mradi huo na shehena yote ipo tayari.


No comments:

Post a Comment