Pages

Sunday, June 30, 2013

OBAMA ANASIMULIZI GANI KUHUSU AFRIKA?

Obama ana simulizi mbaya ya Afrika kichwani mwake

 
Imeandikwa, imewasilishwa na Maggid Mjengwa--

BARACK Obama ametua Afrika. Mguu wake wa kwanza ameukanyagia Senegal. Neno lake kuu akiwa Senegal ni DEMOKRASIA. Ameisifu Senegal kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kukuza demokrasia barani Afrika.

Kisha ametua Afrika Kusini. Jana Jumamosi ametembelea Kisiwa cha Robben, mahali ambapo Nelson Mandela alifungwa kwa miaka 27. Inahusu DEMOKRASIA. Bila shaka, Obama ataisifu Afrika Kusini kwa kukuza demokrasia yake na hivyo kuinua uchumi wake. Maana, pasipo na demokrasia ni nadra kwa uchumi kukua.

Kesho Barack Obama atatua Dar Es Salaam, Tanzania. Huhitaji kuwa mtabiri, kujua , kuwa Barack Obama atalitamka neno DEMOKRASIA akiwa Tanzania. Huenda Obama akaitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa katika kudumisha Amani na Umoja miongoni mwa watu wake. Lakini, bado Obama atasisitiza pia umuhimu wa demokrasia na uhuru zaidi wa vyombo vya habari barani Afrika.

Obama anaipenda Afrika, ni bara alilozaliwa baba yake mzazi, Dr. Barack Hussein Obama, Sir. Hivyo, kwa Barack Obama, Afrika ni bara la asili yake, na Kenya ndiko iliko asili yake. Ndiko liliko kaburi la baba yake.

Lakini, Obama ana simulizi mbaya juu ya bara hili.....

Soma zaidi: mjengwablog.com


Source: http://www.wavuti.com

KAMA NI MWANAUME NA UNASHIRIKI TENDO LA NDOA SOMA HII


Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.

Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.

Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujam

iiana. 

Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.

Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.

"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.

“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.

Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….

Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……
Source: Jamii Forums

MAAJABU HAYA NYATI AJIFUNGUA 'BINADAMU'

Unbelievable+Human-like+Buffalo+BirthNchini Thailand, Nyati  amezaaa mtoto anayefanana sana na mwanadamu. 

Hizi ni picha ya nyati zikionyesha uso  na wa binadamu hasa yake ambayo ni sawa . Hata hivyo, mikono yake na miguu inafanana  zaidi na  nyati. Lakini kwa ujumla nyati anafanana sana na ng’ombe, Lakini sio kwa binadamu.


Kwa bahati mbaya kiumbe huyu alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa. 

Hli jambo limeleta gumzo na mtafarukiu mkubwa katiak kijiji hicho kuna imani kwamba tukio kama hilo linata baraka kwa watu wote wa sehemu tukio lilipotokea.

kutokana na imani hii watu wengi wameonekana wakiomba na kusali ili wapate baraka. uso wa kiumbe  huyu huwezi kutofautisha ni binadamu au ni nyati alisikika mwanakijiji mmoja.
 
 
 
Via/jumamtandablog

RAIS OBAMA AKITOKEA SAUZ, DAR YAPAMBAMOTO

Wakazi wa Dar es salaam wameendelea kuona nguvu za ulinzi wa Rais wa Marekani, Barak Obama kuanzia Baharini, angani na katika vyombo vya habari. Angalia picha hiyo kama kielelezo sahihi za kudhihirisha wanachomaanisha.

RAIS OBAMA NA MKEWE WATOKELEZEA KIZULU

VAZI LA KIZULU, limewapendezaje?
Rais Obama akiw na mkewe wakiwa wanafurahia vazi l kiasili la kizulu:

Saturday, June 29, 2013

RAIS OBAMA AMZUNGUMZIA MZEE MANDELA


Rais Barak Obama amesema Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Mzee Nelson Mandela ameonyesha Uvumilivu na ujasiri na kwamba ni mtu wa kuigwa duniani.

Rais wa Marekani Barack Obama, amesema uvumilivu na ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na upendo wa dhati wa rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni kwa namna gani alivyo na utu wa kibinadamu.

Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha ukweli na ukakamavu ambao una maana kubwa katika utu wa kibinadamu ambao uliondoa tabaka la ubaguzi, udini na utaifa.

Rais huyo wa Marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria baada ya mazungumzo na rais wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
 
via/jumamtandablog

KIKAO CHA WABUNGE WA CCM DODOMA

IMG_0004Mkurugenzi wa Idara ya mambo ya Nje ya CCM, Dr.Asha Rose Migiro akikaribishwa na Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha wabunge wa CCm Juni 29, 2013. Katikati ni Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)IMG_0012Katibu Mkuu, wa CCM, Abdlrahman Kinana akiongozwa na Katibu wa wabunge wa CCM, Jenista Mhagama kuingia kwenye ukumbi wa Msekwa  mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha wabunge wa CCM juni 29, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)IMG_0010Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje ya CCM, Dr Asha Rose Migiro akisalimaina na Mbumge wa Kondoa Kusini wakati alipowasili kwenye ukumbiu wa Msekwa mjini Dodoma Juni 29, kuhushuria kikao cha wabunge wa CCM.  Katikati ni Mbunge wa Mpwapwa  ns Nsibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory heu;(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0043Wabunge wa CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wao, waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozungumza katika kikao chaokwenye ukumbiwa Msekwamjini Dodoma Juni 29, 2013. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0030Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wabunge wa CCM wakiimba wimbo wa CCM kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa msekwa mjini Dodoma Juni 29, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri MkuuIMG_0052Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wabunge wa CCM wakiimba wimbo wa CCM kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa msekwa mjini Dodoma Juni 29, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri MkuuIMG_0019Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha wabunge wa CCM Juni 29, 2013. Kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

ZIARA YA MKUU WA MAJESHI MWAMUNYANGE NCHINI OMAN

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akikagua Gwaride la Mapokezi mara alipowasili katika Makao makuu ya Jeshi la Oman kuanza Ziara ya kikazi nchini Oman, kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Oman Luteni Jeneral Ahmed bin Harith Al Nabhani.
Mkuu wa Majeshi akiwa katika mazungumzo na Mwenyeji wake.


Mku wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  katikati) akiwa katika mazungumzo na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mhe. Sultan bin Mohamed Al Nuam ani (kulia), akishuhudia ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh (kushoto)

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  akipokea taarifa kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi Ali  Ahmed Saleh alipotemb elea ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh akimuonyesha Mkuu wa Majeshi mchoro wa litakalokuwa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh mstari wa mbele kulia akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa majeshi na ujumbe wake.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Uongozi na kamandi  cha Oman.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  akisalimiana na Meja Saif Wibonela, Mwanafunzi wa kitanzania anaesoma hapo.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  (watano kutoka kushoto waliokaa ) katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Anga  cha Oman (watatu kutoka kushoto waliokaa) ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi Ali Ahmed Saleh.



Mkuu wa majeshi ya Tanzania Jenerali  Davis Mwamunyange, alifanya ziara ya Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 23 hadi 27 Juni 2013 kwa Mwaliko wa mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani.


Ziara hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa kindungu uliopo baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya ulinzi na kuanzisha uhusiano wa karibu na ushirikiano baina ya vyombo hivi vya ulinzi kati ya Tanzania na Oman.

Katika ziara hii Mhe. Jenerali Mwamunyange alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani na pia kukutana na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mheshimiwa Luteni Jenerali Sultan bin Mohamed Al Nuamani .

Mbali na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mkuu wa majeshi alipata nafasi kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli mbalimbali za Jeshi la Oman, alitembelea makumbusho ya Jeshi la Oman, Chuo cha Uongozi na kamandi cha Oman, Chuo cha Jeshi la Anga, Hospital ya Jeshi , Makao makuu ya Jeshi la Askari wa Miguu pamoja Makao makuu ya Jeshi la Majini.

Katika maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Mkuu wa Majeshi alifurahishwa sana na shughuli za jeshi la Oman na kuridhika na hatua iliyopigwa na Jeshi la Oman. Mkuu wa majeshi pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi.

Friday, June 28, 2013

MASANGOMA WAINGIA KAZINI, WAFANYA TAMBIKO KWA NIA YA KUMUOKOA MANDELA ANAYEPUMULIA MASHINE

 
Sasa ni dhahiri kuwa maisha ya kiongozi wa zamani wa nchi hii, Nelson Mandela yamo hatarini kutokana na kwamba anaishi kwa msaada wa mashine, imethibitishwa na mmoja wa wazee wa ukoo wa kiongozi huyo.


Binti yake mkubwa Makaziwe naye amethibitisha hilo, akisema hali ni mbaya na chochote chaweza kutokea.
 
"Naweza kusisitiza hilo, kwamba Tata (baba) hali yake ni mbaya sana, chochote chaweza kutokea, lakini nataka nisisitize tena, kwamba ni Mungu tu ndiye anajua muda wa kuondoka,” alikiambia kituo cha utangazaji cha SAFM jana.
 
Hali hiyo inayotia mashaka imesababisha hata Rais Jacob Zuma afute safari yake ya Msumbiji ambako alipanga kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
 
“Ndiyo, anatumia mashine kupumua,” Mzee Napilisi Mandela aliiambia AFP muda mfupi baada ya kumtembelea Mandela hospitalini juzi. “Hali ni mbaya, lakini tutafanyaje.”
 
Zuma alifuta safari yake iliyokuwa ifanyike jana baada ya “kubaini, kwamba kiongozi huyo wa zamani hali yake bado ni mbaya,” taarifa kutoka Ofisi ya Rais ilisema.
 
Wakati huo huo, kiongozi wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-moon alisema juzi kwamba dunia yote inamwombea Mandela wakati huu ambapo anapigania maisha yake.
 
Ban alimwita Mandela “mmoja wa mashujaa wa karne ya 20” katika hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika, OAU (sasa Umoja wa Afrika-AU) iliyofanyika New York, Marekani, ambao uliongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. 
 
“Najua fikra na maombi yetu viko na Nelson Mandela, familia yake na wanaompenda, Waafrika Kusini wote na watu wote duniani ambao wamekuwa wakivutiwa na matendo yake maishani na kuwa mfano wa kuigwa,” alisema Ban. 
 
“Hebu nasi leo tuoneshe dhamira ya uwajibikaji wa dhati katika kuhakikisha tunaboresha maisha na fursa za Waafrika wote,” alisema Katibu Mkuu wa UN. 
 
Zuma alimtembelea Mandela hospitalini juzi saa nne usiku na kumkuta akiwa bado na hali mbaya, msemaji wa Rais, Mac Maharaj alisema. 
 
“Rais Zuma alizungumza na madaktari ambao bado wanaendelea kufanya kila linalowezekana kuokoa maisha yake ... ameamua kufuta safari yake ya Maputo kesho (jana), ambako alitakiwa kuhudhuria Mkutano wa Uwekezaji katika miundombinu kwa nchi za Kusini mwa Afrika wanachama wa SADC.”
 
Mandela (94) alilazwa katika hospitali ya moyo ya Medi-Clinic iliyoko hapa Juni 8 kutokana na kuibuka upya kwa matatizo ya mapafu yake. 
 
Katika hatua nyingine, mjukuu wake, Mandla Mandela, amekanusha kuwapo kwa mvutano kati yake na shangazi yake, Makaziwe, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana.
 
Magazeti yaliripoti juzi kwamba anadaiwa alijitoa kwenye kikao cha familia kilichofanyika Qunu Jumanne. 
 
Kwa mujibu wa taarifa hizo, anadaiwa kuhamisha makaburi ya watoto watatu wa Mandela kutoka Qunu hadi Mvezo mwaka 2011, bila hata kushauriana na familia. 
 
Iliripotiwa pia kuwa familia hiyo ilikuwa ikitaka watoto hao, Makgatho, Thembekile na Makaziwe, warudishwe Qunu.
 
“Chifu Zwelivelile (Mandla) hana suala lolote na mtu mwenye mamlaka ya kurudisha Qunu kaburi lolote au makaburi yote,” msemaji wa Mandla, Freddy Pilusa alikaririwa akiiambia The Star jana.
 
“Mvezo ndiko mahali ilikozaliwa familia ya  Mandela na kimila ndiko nyumbani kwao, na hivyo ndiko iliko historia ya familia hiyo.” Alisema Mandla hawezi sasa kuzungumzia lolote kuhusu mipango ya maziko ya babu yake. 
 
Waganga wa jadi wa Limpopo jana walifanya matambiko katika ofisi za ANC zilizoko Polokwane kumwombea Mandela.
 
Mwenyekiti wa Timu kazi ya ANC Limpopo, Falaza Mdaka, alisema waganga hao waliomba kufanyia tambiko lao katika ofisi hizo wakisema ndiko kulikuwa ‘nyumbani’ kwa Mandela na kuongeza kuwa alikuwa mtu wa aina yake na dunia bado inamhitaji. 
 
Waganga hao waliimba nyimbo za mapambano na kuchoma ubani, wakiwaomba wahenga kumponesha kiongozi huyo anayependwa na nchi nzima.
 
“Mandela anahitaji msaada wa wahenga,” alisema mmoja wa waganga hao, Sylvester Hlathi.
Via/jumamtanda blog

MKWARA MZITO UJIO WA OBAMA DAR.



DAR ES SALAAM.  
MAKACHERO wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatar
ajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana na Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja aliliambia gazeti hili kuwa helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu, ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.
Inaaminika kuwa helikopta hizo zitakuwa zinasaidia kusafirisha watu na mizigo kutoka kwenye meli za kivita ambazo zimeegeshwa kwenye Kikosi cha Maji cha JWTZ.
Pia helikopta mbili zinaaminika ziko katika meli ambazo zimeegeshwa huko Kigamboni.
Meli za kivita na ndege ya kijeshi
Katika hatua nyingine, meli mbili za kivita ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu zimeegeshwa Kigamboni.
“Jamaa wana meli kali kwa kweli, mimi nimekuwa askari wa Kikosi cha Maji kwa muda mrefu na kufanya mazoezi na mataifa kadhaa, lakini sijaona meli kama zile.
CHANZO MWANANCHI

MAGAZETI YA IJUMAA 28/6/2013 NA YALIYOCHOMOZA

Soma Magazeti ya Ijumaa 28/6/2013 na yaliyochomoza zaidi Ubabe wa Marekani kumlinda Rais Obama  katika ziara yake nchi za Afrika hususani Tanzania na Giza nene lililotanda Afrika Kusini, Afya ya Mandela (Mzee Madiba) 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Thursday, June 27, 2013

DU SIKU ZA UTUMWA BAGAMOYO, WATUMISHI WA UCHAPAJI WIZARA YA ELIMU WATOA MACHOZI

 Mhariri Msaidizi wa Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini Bw. Juma Nyumayo (kulia) akishika pembe ya ndovu iliyobebwa na sanamu ya Mtumwa iliyojengwa mbele ya jingo mlango wa kuingilia Caravanserai. Hapo ni Hoteli ya wafanyabiashara wa masafa marefu ya watumwa ijulikanayo kama Caravanserai jengo lililopo katika mji wa kihistoria na maendeleo  ya kuanza kwa shule, huduma za afya na biashara za kila aina ikiwa ni pampja na biashara ya Utumwa hapa Tanganyika, (sasa Tanzania) na Afrika ya Mashariki. Picha hii imepigwa Jumatatu 24/6/2013 wakati watumishi wa Uchapaji, Vituo vya Uchapaji Kanda na Kituo cha Kisomo Mwanza ambao wapo chini ya Idara ya Elimu ya Watu Wazima, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walipotembelea maeneo ya Historia ya Mji huo kwa lengo la kujifunza uhifadhi wa majengo na historia ya maeneo hayo kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho hapa ulimwenguni. 

Mlango mmojawapo uliotengenezwa kwa ujuzi na wachongaji wasanii wa Enzi hizo uliotumika na wafanyabiashara wa kiarabu waliojihusisha na biashara ya utumwa huko Bagamoyo, Tanzania bila kushau maliasili ikiwa ni pampja na meno ya ndovu.

Hayo majengo ya Enzi hizo bado yapo, na hapo ni moja ya mtaa mashuhuri wa kibiashara katika Mji wa Bagamoyo (bonge ya Street) enzi hizo ambapo ni matajiri tu w biashara ya utumwa waliweza kumiliki majengo hayo na kurandaranda katika mitaa huku wakijipongeza kwa kunywa kahawa na kula  tende baada ya kufanikiwa kibiashara ambayo ilichukua masafa marefu kwa kuwauza binadamu ambao waliuzwa kama mihogo na kuilinganisha kwa ukubwa na ubora na wakati mwingine mfanyabiashara aliweza kupata nyongeza ya mtumwa mdogo dhaifu kama wafanyavyo kwenye ndizi endapo amemnunua mtumwa mwenye nguvu nyingi umbile kubwa kwa bei kubwa. Hapo baadhi ya kazi za sanaa za mikono kama kuchonga, kuchora , kufinyanga na nyinginezo zinauzwa kama unavyoziona katika picha hii sasa. 


Ni Mtaa mmojawapo wa kale hapo mjini Bagamoyo


Soko kuu la kale hapo Bagamoyo mpaka sasa linatumika kwa kuuza kazi za sanaa kwa watalii wa ndani na nje kama inavyoonekana

Ndani ya Jengo la Caravan sarai kuna makumbusho ambayo inaonesha picha mbalimbali za majengo ya kanisa misikiti ya utawala shule na wavumbuzi waliowahi kupita hapo Bagamoyo kama Dr Livingstone na wengine kibao. Hapo Mtumishi wa Kiwanda cha Uchapaji Press 'A' Lukia akiangalia picha hizoo ndani ya chumba cha makumbusho katika jengo la Caravanserai.
 

 

Mhariri wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yenye makao yake Makuu Mbeya, (kulia) akipiga picha kisima cha kale huku baadhi ya watumishi wakiangalia  na kusikiliza maelezo toka kwa kijana muongoza watalii hayupo pichani.
 
 
 
 
Kijana Muongoza watalii (aliyevaa T-shirt kushoto) akiwapa maelezo baadhi ya watumishi wa Uchapaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu kisima cha maji cha kale ambacho kinatumika mpaka leo ndani ya jingo la Caravanserai mjini Bagamoyo. Picha zifuatazo ni makundi mengine yakipewa pia maelezo kuhusu kisima hicho.