Pages

Tuesday, May 14, 2013

SONGEA KUMEKUCHA, MAVUNO NA BIASHARA


Shehena ya Mahindi ikishushwakatika Soko la SODECO lililopo Manispaa ya Songea,  toka kwa wakulima wa Kijiji cha Mgazini Kata ya Kilagano, Songea Vijijini leo (Picha na Juma Nyumayo)


Kazi inaendelea, baridi na jua kwa mbali, Soya ikimwagwa kuangalia ubora wake kabla ya kupimwa upya.
( samahani kwa ubora wa picha iliyoingiliwa na mwanga wa jua la asubuhi.)


Wafanya biashara wakimwaga Soya tayari kwa kupima upya hapo SODECO Manispaa ya Songea.
  Soko hilo linalomilikiwa na Halamashauri ya wilaya Songea vijijini na kwamba hivi sasa limechangamka kama lilivyoonekana leo. 


Mahindi yakimwagwa tayari kwa kupimwa na kuwekwa katika viroba kwa kipimo maalum kusafirishwa nje ya mkoa wa Ruvuma


Pilikapilika katika Soko la Mazao Mchanganyiko, SODECO Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo.


Kazi ya Ukaguzi wa mahindi kabla ya kupima upya na kufunga katika viroba ikiendelea na wafanyabiashara wa SODECO leo


No comments:

Post a Comment