Pages

Wednesday, May 8, 2013

RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA BOMU LA ARUSHA

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Joachim Assey (aliyekaa kushoto kwake) wakati akihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Mama Salma Kikwete akipungia wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha Mei 7, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa  msichana Patricia Joachim Assey (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu  katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na  mlipuko wa bomu jumapili iliyopita Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia
ya Olasiti. jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake  rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa
mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa  pole kwa watawa wa kanisa hilo wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa  Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat  Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi  katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana  pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa  kijana James Gabriel (16) aliyefariiki katika shambulio la kigaidi
katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha
Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment