Pages

Sunday, May 26, 2013

MBOWE ATEMA CHECHE, WATU KIBAO WAMSHANGILIA MKUTANO WA KANDA SONGEA






Mwenyekiti wa Chana cha Chadema - CDM - Taifa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe Freeman Mbowe, (Mb.)  akihutubia umati wa watu katika viwanja vya Shule ya Msingi Matarawe manispaa ya Songea wakati wa kampeni ya Chama hicho kuzindua kanda ya kusini leo. (Picha na Juma Nyumayo)


Mhe. Freeman Mbowe,  akisisitiza umuhimu wa wananchi wa mikoa ya Kusini, hasa mkoa wa Ruvuma ambao hauna Mbunge wa Upinzani hata mmoja kujiunga na vita ya kupambana na ufisadi na kunyimwa haki wananchi kwa kujiunga na upinzani katika viwanja vya Shule ya Msingi Matarawe Manispaa ya  Songea leo.


Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kusikiliza mkutano wa uzinduzi wa Kanda ya Chadema Kusini  mwa Tanzania mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma leo ambapo Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho alihutubia.


Nidhamu kwa kwenda mbele watu wa makundi na rika tofauti wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe, katika Mkutano wa kihistoria wa Kufungua kanda ya chama hicho uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Matarawe leo.


Mpambe wa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, (mwenye nguo ya mabaka meusi) aliyesimama nyuma ya kiongozi huyo, akiwa makini kuangalia usalama wakati akihutubia wananchi  katika viwanja vya shule ya Msingi Matarawe leo kuhusu vita dhidi ya mafisadi na umuhimu wa wananchi hao kujiunga na Chadema. Chama hicho kimekamata kata tano nafasi za udiwani Jimbo la Songea mjini zikiwa ni Kata ya majengo, Misufini, Mfaranyaki, Bombambili, Lizaboni na Bombambili. Mkutano huo uliopigwa marufuku na baadae kuruhusiwa kwa hekimas za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhe Said Thabit Mwambungu kutokana na  kukubaliana na vingozi wa Chadema kutofanya maandamano.
Tendo hilo limewafanya chadema leo kumsifu mkuu wa mkoa huyo hadharani kwa maauzi yake. (Picha na Maelezo yote na Juma Nyumayo)


No comments:

Post a Comment