Pages

Wednesday, May 29, 2013

DKT. NCHIMBI AWAONDOA HOFU WANANCHI NA RAIA WA KIGENI, ASISITIZA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA NCHINI


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na mmojawapo wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya waliofanya kikao naye jijini Dar es Salaam  Katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Kikao na Wawakilishi wa Nchi za Umoja wa Ulaya waliomtembelea Wizarani..  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema, pia alihudhuria Kikao hicho akiwa na Wakuu wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam (Kushoto).Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
---
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel nchimbi amesema Serikali imeimarisha shughuli za ulinzi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa wananchi na wageni wanaishi na kufanya shughuli zao kwa amani.

Dk. Nchimbi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Ujumbe wa wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na baadhi ya mabalozi wa Nchi hizo waliopo hapa nchini.
Aliuambia ujumbe huo ulioongozwa na Balozi Filberto Cerani Sebregondi kuwa Jeshi la Polisi limeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

Amesema kwa upande wa raia wa kigeni, Jeshi hilo limeanzisha Dawati Maalumu litakalohudumia raia hao pale wanapopata matatizo ili waweze kupata huduma za haraka.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe huo  amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na ameishukuru Wizara hiyo kwa jitihada inazoendelea kuchukua kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa wageni na raia

No comments:

Post a Comment