Pages

Sunday, May 12, 2013

DIAMOND AFANYA KWELI UINGEREZA, AWA MSANII WA KWANZA WA KIBONGO KUUZA WIMBO KAMPUNI YA SIMU

WAKATI baadhi ya wasanii wakijitoa katika mikataba ya kuuza miito ya nyimbo zao kwenye Makampuni ya Simu, Msanii maafuru ndani na nje ya nchi Naseeb Abdul Diamond amekuwa msanii wa kwanza kupata mkataba wa kuuza nyimbo zake kwenye miito ya simu nchini Uingereza.

Diamond ambaye ndiye msanii pekee wa bongo fleva anaelipwa pesa nyingi nchini kutokana na mauzo ya nyimbo zake katika miito ya simu (caller tune), amesema kwamba miito hiyo ya simu itaongeza mauzo ya kazi zake na kwamba watanzania wanaoishi nchini humo pia watapata fulsa ya kusikiliza nyimbo zake kila wakati. 
 
Mwanamuziki huyo wa Bongo Fleva amepata dili hilo kubwa la kuuza miito hiyo ya simu na kuwa msanii wa kwanza nchini kujipatia kitita kikubwa cha fedha kupitia nyimbo zake(caller tune) Nchini Uingereza. 
Dili hilo limeonyesha kumfurahisha sana Diamond kwani tayari anaamini kuwa kazi anayoifanya ni nzuri na inaweza kusikilizwa na watanzania waishio Uingereza na Waingereza pia kwa kununua miito ya simu wakiwa nnchini humo. 
 
Msanii huyo anajivunia suala hilo kwa sababu itawezesha watanzania waishio nchini Uingereza kupata nyimbo zake kwa wakati unaotakiwa tofauti na ilivyo sasa. 

Diamond Platinum ambaye hivi karibuni alikumbwa na kashfa ya kudanganya umma kuwa mpenzi wake wa sasa ambaye ni mtangazaji wa Runinga katika kituo cha DTV Peniel Mungilwa 'Penny' ni mjamzito wa miezi mitatu alikuwa nchini humo kwa ziara ya kisanaa. 

Hata hivyo mwana dada huyo alikanusha taarifa hizo na kudai kwamba hana ujauzito wa msanii huyo na kwamba hajawai kubeba ujauzito wake

No comments:

Post a Comment